Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 6, 2020

TRA Yashauriwa Kuendelea Kuwekeza Kwenye Teknolojia Ya Kisasa

juu
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeshauliwa kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa kwa kuwa Tanzania ni nchi mojawapo za ukanda wa Afrika Mashariki yenye lango kuu la kuingilia ukanda huo suala linalosaidia kukuza uchumi kupitia ushuru wa forodha unaotozwa katika eneo hilo.

Ushauri huo umetolewa jana na Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya alipotembelea TRA akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini

“Ili kusimamia ushuru wa forodha ipasavyo, suala la teknolojia halikwepeki, hivyo ni muhimu TRA ijikite zaidi katika kuendelea kuwekeza kwenye mifumo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na watumishi wenye uwezo wa kuendesha mifumo hiyo,” alieleza.

Dkt. Kunio Mikuriya alisema kwamba, akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede, wamezungumzia juu ya umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kudhibiti na kusimamia ushuru wa forodha kwenye bandari ya Dar es Salaam na maeneo mbalimbali hapa nchini.

Naye, Kamishna Mkuu wa TRA alisema kuwa, ziara ya Katibu Mkuu huyo imelenga kuimarisha mahusiano baina ya nchi wanachama wa WCO ambapo ametokea nchini Kenya kwa ajili ya kazi hiyo pia.

“Tanzania ni mwanachama wa WCO na kuna mashirikianio ambayo tunafanya kwa pamoja kuhakikisha eneo la forodha linatekeleza majukumu yake ili kuhakikisha kuna usalama wa bidhaa kwenye eneo la biashara,” alisema Dkt. Mhede.

Alisema kuwa, Tanzania ni kitovu cha biashara kwa kuwa inahudumia nchi zote ambazo hazina bandari kwa mfano Zambia, Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao wote wanatumia Bandari ya Dar es Salaam, hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika kusimamia masuala yote ya kiforodha.

Katibu Mkuu wa WCO Dkt. Kunio Mikuriya baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania alielekea jijini Dodoma kwa lengo la kukutana na baadhi ya watunga sera kwa ajili ya kuimarisha mahusiano yaliyopo.

Mwisho.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )