Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 2, 2020

Virusi Vya Ugonjwa Wa Corona Nchini China Washusha Bei Ya Pembe za Ng’ombe Kahama.

juu
SALVATORY NTANDU
Wafanyabiashara wa Pembe za Ng’ombe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wamesema kuwa, kuibuka kwa virusi vya ugonjwa wa corona nchini china umesababisha biashara hiyo kushuka kutoka shilingi elfu 20,000 hadi 15,000 kwa kilo.

Hayo yalibainishwa Januari 31 mwaka huu na mfanyabiashara wa pembe za ng’ombe  mjini kahama, Emmanuel Kitonka, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana  hali ya biashara hiyo  baada ya  wanunuzi mazo yatokanayo na mifugo  kushindwa kuja nchini baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa Corona.

Alisema kuwa kwa sasa wanapata hasara kutokana na kushindwa kusafirisha pembe za ngombe na mazao mengine kama vile sehemu za uzazi za ng’ombe ambazo hapo awali zilikuwa zinanunuliwa kwa bei ya juu ikilinganishwa na hivi sasa.

“Kabla ya kuibuka kwa virusi hivyo,walikuwa wakiuza kilo moja ya sehemu za uzazi za ng’ombe (viungo vya uzazi) chini Tanzania tulikuwa tunauza shilingi elfu 25,000 lakini mpaka sasa bei imeshuka hadi kufikia kiasi cha shilingi 17,000 kwa kilo moja.

Tumepata hasara kubwa kutokana na biashara zetu kushuka na  tunashindwa kuendelea kufanya biashara hii na kama hali hii itaendelea hivi tutashindwa kufanyabiashara kutokana na wanunuzi wengi hutoka nchini china kushindwa kuja Tanzania kununua mazao yatokanayo na ng’ombe katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Nae kaimu  Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya mji wa kahama Dkt, Damiani Kilyenyi alikili kuwepo kwa biashara ya mazao yatokanayo na Ng’ombe(pembe na Viungo vya uzazi) wilayani kahama ambazo hutumika  katika matumizi mbalimbali katika nchi za bara la Asia.

Amefafanua  kuwa, sheria ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo ya namba 17 ya mwaka 2003 hairuhusu viungo vya uzazi vya mifugo kubebwa kwa ajili ya matumizi mengine kwani kunamagonjwa mengine ambayo binadamu anaweza kupata magonjwa mengine kutokana  kushika via vya uzazi vya mifugo.

“Biashara ya pembe za ng’ombe inaruhusiwa kufanyika hapa nchini lakini biashara ya viungo vya uzazi vya ng’ombe  hairuhusiwi kwa mujibu wa sheria za nchi wafanyabiashara wengi wilayani humu wanapenda kuifanya biashara hii kwa siri lakini kwa sasa tunaendelea kuwafuatilia ili tuwachukulie hatua”alisema Dk Kilyenyi.

Kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba viungo vya uzazi vya ng’ombe vinatengenezewa nyuzi za kushonea binadamu Pindi anapopata jeraha na soko lake kuu lipo nchini China ambapo wafanyabiashara hususani wa wilayani kahama wanaifanya biashara hii kwa siri ili maafisa wa serikali wasijue kwa kuogopa kuchukuliwa sheria.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )