Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 28, 2020

Wanajeshi 33 wa Uturuki Wauawa Katika Mapigano Makali Huko Syria

juu
Wanajeshi 33, wa Uturuki wameuawa katika mapigano kwenye mkoa wa Idlib nchini Syria.

Shirika la habari la serikali ya Uturuki, Anadolu, lililomnukuu gavana wa jimbo la Uturuki la Hatay lililopakana na mkoa wa Idlib, Rahmi Dogan imeripoti habari hiyo.

Dogan amesema wanajeshi hao wamekufa katika shambulizi la angani lililofanywa na ndege za jeshi la serikali ya Syria na kuongeza kuwa kulikuwa na wanajeshi waliojeruhiwa vibaya sana na wanaendelea kupatiwa matibabu.

 Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amefanya mikutano miwili ya dharura jana jioni kujadiliana kuhusu hali ilivyo katika mkoa huo wa Idlib. 

Waziri wa mambo ya kigeni, Mevlut Cavusoglu kwa upande wake alijadiliana kwa njia ya simu na katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami barani Ulaya, NATO Jens Stoltenberg, kuhusu hali kwenye mkoa huo hii pia ikiwa ni kulingana na Anadolu.

Katika upande mwingine, vyombo vya habari vimetangaza kuwa vikosi vya jeshi la Uturuki vimeshambulia ngome za jeshi la Syria kaskazini mwa mkoa wa Aleppo (Halab) ndani ya ardhi ya Syria.

Wakati huohuo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema, imetiwa wasiwasi na shambulio dhidi ya jeshi la Uturuki katika eneo la Idlib na kwamba Washington iko bega kwa bega na nchi hiyo kwa kuwa ni mshirika  wake katika shirika la kijeshi la NATO.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )