Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 10, 2020

Wasira amjibu Zitto Kabwe Kuhusu kuzuiwa mkopo wa Benki ya Dunia

juu
Mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira amesema hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuishawishi Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa dola za Marekani milioni 500 kwa Tanzania, siyo jibu pekee la kutatua tatizo la wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni.

Fedha za mkopo huo ambazo ni zaidi ya Sh1.2 trilioni zingeelekezwa katika kushughulikia programu za elimu nchini zikiwemo kujenga miundombinu ya madarasa na ununuzi wa vifaa vya kufundishia.

Hata hivyo, Zitto na wanaharakati wa Tanzania na wa kimataifa waliishinikiza benki hiyo isitoe mkopo huo kwa Serikali kutokana na kile walichokiita kuwa ni sera na sheria ya elimu ya kibaguzi kwa wasichana wanaotapata mimba wakiwa shuleni.

Wasira aliyekuwa akizungumza leo (Februari 10, 2020) katika kipindi cha Clouds 360 cha televisheni ya Clouds, amesema kupata mimba ni changamoto ya jinsia na msingi wa nchi ni kusomesha watoto wote bila kuwabagua na lazima nchi iangalie namna ya kumaliza tatizo la mimba kwa wasichana waliopo shuleni.  

Wasira amesema alimsikiliza Zitto walipohojiwa mjini Washington DC, Marekani na  aliwasikiliza na Watanzania wanasemaje kuhusu hoja hiyo.

Yupo Mtanzania mmoja anaitwa Salma alimuuliza Zitto swali hili, “lakini wewe (Zitto) sasa unataka benki isitoe mkopo, kwa kufanya hivi si unawaumiza Watanzania wengi zaidi kuliko kuwasaidia, inasaidia nini?”

Wasira amesema katika majibu yake Zitto amesema, “ilani (ya CCM)  ilisema wakipata mimba wasome.”


Waziri huyo wa zamani akieleza mtazamo wake kuhusu majibu na hoja ya Zitto amesema, “mimi ningekuwa kijana kama Zitto ningemjibu na hata kama mimi sio kijana ninaweza kumjibu kwa sababu hoja zake zinajibika.”

 “Msingi wetu ni kusomesha watoto, kupata mimba ni changamoto inayotokana na gender (jinsia), nafikiri watu wazima ambao lengo letu ni kuwasomesha watoto wote lakini ipo changamoto, kuzuia pesa kutoka benki ya dunia sio jibu.

“Mimi ningefikiri vijana wote wangekaa chini pamoja na Zitto tuseme benki lazima itupe pesa lakini tutazame ili tusaidie wasichana wanaopata mimba tunawasaidiaje, kuwaambia tu mtarudi shule sio jibu peke yake, ila inatakiwa kuwasaidia kutopata mimba kwa hiyo benki itupe pesa ili tuwajengee hosteli, maeneo ambako tumejenga hosteli mimba zimepungua
 

“Si wanataka kuwatengenezea watoto wa sekondari, kwa hiyo watupe pesa ili tuwajengee hosteli. Sisi kama chama kikubwa cha siasa hatuwezi kuwaambia watoto zaeni tu, kujenga nchi ni pamoja na kujenga tabia.

"Tunatakiwa kuwaambia wasichana someni na kuwajengea mazingira yanayowapa unafuu, mfano usafiri msichana anapotembea kwa miguu hata lifti ya baiskeli inaweza kuwa kishawishi cha kupata mimba.

“Hoja hapa ni kuweka miundombinu mizuri ili wasipate mimba, lakini anachozungumza Zitto ni kama kuwaambia zaeni tu.”amesema Wasira.

 
Baadhi ya vijana na wanasiasa walishauri Zitto achukuliwe hatua za kisheria  kwa sababu hatua yake kuishawishi Benki ya Dunia isitoe mkopo ni kukosa uzalendo kwa nchi yake.

Lakini kwa upande wake Wasira aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunda Mjini mkoani Mara amesema Zitto alikuwa na hoja zake na zimekubaliwa na Benki ya Dunia na hapaswi kushambuliwa binafsi lakini anatakiwa ajibiwe hoja zake.

Amewataka vijana kujenga utamaduni wa kujibu hoja na kuepuka mashindano yasiyo na tija hasa yale yanayohusu uchama kila linapokuja suala lenye maslahi ya kitaifa.

"Tusikilize hoja na tujibu hoja. Yule mwenye hoja tuachane naye tusikilize unachosema halafu tumjibu. Kama wewe una hoja na sikubaliani na wewe, nitaachana na wewe lakini nitasema hoja yako si sawa.

“Tusijibu tumekasirika, unajua hasira ni wazimu fulani hivi na ukipata wazimu wa hasira unapoteza mwelekeo wa kutoa sababu,” amesema Wasira.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )