Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 20, 2020

Wawili Wafariki kwa Virusi vya Corona Iran

juu
Iran imethibitisha vifo vya watu wawili vilivyotokana na maambukizi mapya ya virusi vya Corona na kuvifanya kuwa vifo vya kwanza kuripotiwa eneo la Mashariki ya Kati. 

Maafisa wa afya nchini Iran, wamesema wanaume wawili wazee wamefariki dunia katika mji wa Qom.

 Shirika la habari la Iran IRNA, limesema shule na vyuo huenda vikafungwa katika mji huo wa Qom kwa ajili ya kufanya uchunguzi. 

Kwingineko watu tisa wameripotiwa kuwa na maambukizi ya Corona katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

 China imeripoti kuendelea kupungua kwa kasi ya maambukizi hii leo na kuweka matumaini ya kumalizika kwa mripuko huo, huku Japan ikikosolewa kutokana na abiria wawili waliokuwamo ndani ya meli iliyowekwa chini ya karantini kufariki. 

Idadi ya vifo ndani ya China bara imefikia watu 2,118 baada ya watu wengine 114 kufariki dunia.

 Zaidi ya watu 74,000 wameambukizwa virusi hivyo ndani ya China na mamia wengine katika nchi zaidi ya 25.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )