Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, March 10, 2020

CHADEMA, Polisi wavurugana Mahakamani

Vurugu na kurushiana maneno vimeibuka  kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakati wa kusikiliza kesi ya viongozi wa Chadema. 
 
Hayo yote ni baada ya polisi kujaribi kuzuia baadhi ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuingia katika chemba za mahakama hiyo kwa ajili ya kusubiri  hukumu ya viongozi wa chama hicho.

Polisi walilazimika kuwazuia wafuasi hao kwa maelezo, kwamba chumba cha mahakama hiyo kimejaa kutokana na watu kuwa wengi.

Kutokana na wafuasi wa Chadema kutokuwa tayari, lakini pia kujiridhisha kwamba nafasi ya kutosha ipo, waliendelea kuwa na msimamo wa kutaka kuingia ndani.

Kutokana na mvutano huo, polisi walilazimika kuruhusu baadhi ya wafuasi hao kuingia huku wengine wakibaki nje.

Leo tarehe 10 Machi 2020, mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya uchochezi Na. 112/2018 inayowakabili viongozi wa Chadema.

==>>Tazama hapo chini
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )