Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 12, 2020

Kambi Ya Jeshi la Marekani Nchini Iraq Yashambuliwa kwa Makombora, Watatu Wafariki

juu
Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa askari wake wawili wameuawa katika shambulizi la maroketi dhidi ya kituo chake nchini Iraq. 

Askari hao wawili wa Marekani na mhudumu mwingine kutoka Uingereza wameuawa katika shambulizi hilo dhidi ya kambi ya Taji, kaskazini mwa Iraq, huku wengine 12 wakijeruhiwa. 

Kambi hiyo inayotumiwa na muungano wa nchi kadhaa za Magharibi zikiongozwa na Marekani  imeshambuliwa kwa makombora 18 jana.

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa miongoni mwa watu hao 12 waliojeruhiwa, wanajeshi watano wamejeruhiwa vibaya na wameondolewa kutoka katika kambi hiyo. 

Kuna uwezekano wa idadi ya vifo kupanda kwasababu ya majeraha waliyopata baadhi ya wanajeshi. 

Rais wa Iraq ameshutumu shambulio hilo dhidi ya kambi ya jeshi, akitoa wito wa uchunguzi kuhusiana na shambulio hilo. 

Katika taarifa, ofisi ya rais imeongeza kuwa mashambulizi haya yanalenga usalama wa Iraq.
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )