Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 5, 2020

Kenya Kuwaondoa Wanajeshi wake Somalia

juu
Kenya inatarajia katika siku kadhaa zijazo kuanza mjadala wa kuondosha vikosi vyake katika mpango wa amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (Amisom). Jeshi la Kenya limekuwa likihudumu nchini Somalia kwa miaka 8.

Hatua hiyo inatarajiwa kuchukuliwa baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa tamko la onyo kali saa chache zilizopita dhidi ya Somalia kuhusu kile alichokiita uingiliaji wa mamlaka ya maeneo ya nchi yake.

Hatua hiyo itakuwa ni kukifikisha mwisho kipindi cha takribani miaka minane ya jeshi la Kenya KDF lililoingia Somalia kwa lengo la kukabiliana na kundi la al-shabaab nchini Somalia.

Katika kile kinacholezwa kutokea Jumatatu iliyopita, serikali ya Kenya imesema jeshi la Somalia lilivuka mpaka na kuharibu mali za Wakenya katika mji wa Mandera, ambao upo mpakani na Somalia.

Hata hivyo waziri wa habari wa Somalia hakuweza kupatikana mara moja kujibu malalamiko ya Kenya.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )