Serikali ya Hispania imesema kuwa Mke wa Waziri Mkuu, Pedro Sanchez amethibitika kuwa na virusi vya corona.
Serikali ya nchi hiyo imesema kuwa Waziri Mkuu huyo na mke wake wanaendelea vizuri na wanaendelea kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya wakiwa nyumbani.
Hispania imeweka marufuku ya karibu nchi nzima inayowazuia watu kuondoka majumbani isipokuwa kwa lengo la kwenda kazini, kutafuta matibabu au kununua chakula.
Maradhi ya COVID-19 tayari yamesababisha vifo vya watu 196 nchini Uhisapania na kulifanya kuwa taifa lililoathiriwa zaidi na virusi hivyo barani Ulaya baada ya Italia.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )