Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, March 11, 2020

Rais Vladmir Putin aunga mkono marekebisho ya katiba ya Urusi Yatakayomfanya Agombee Tena Urais

juu
Rais Vladmir Putin wa Urusi amesema anaunga mkono pendekezo la marekebisho ya katiba yatakayomfanya abakie madarakani hadi mwaka 2036 baada ya kipindi chake kumalizika 2024

Putin ameunga mkono mapendekezo hayo yaliyowasilishwa na mbunge ambaye wakati wa utawala wa Soviet alikuwa mwanamke wa kwanza kusafiri anga za mbali. 

Mbunge huyo amependekeza ama iondolewe kabisa sheria ya ukomo wa muhula wa rais madarakani au pafanyike marekebisho ya katiba yatakayomruhusu Putin agombee tena. 

Msururu wa marekebisho ya katiba ya Urusi yatapigiwa kura nchi nzima mnamo tarehe 22 mwezi Ujao wa Aprili. 

Rais Putin ameipinga hatua ya kuondolewa ukomo wa muhula wa rais lakini ameunga mkono fikra ya kufanyika marekebisho ya katiba.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )