Saudi Arabia imesema leo itasimamisha safari zote za ndege za kimataifa kwa wiki mbili, ikiwa ni sehemu ya jitihada za taifa hilo katika kudhibiti usambaaji wa mripuko wa virusi vya corona.
Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa hilo SPA, likinukuu chanzo kutoka wizara ya mambo ya ndani, ambacho halikukitaja, hatua hiyo imepangwa kuchukuliwa kesho kuanzia saa tano Asubuhi.
Tangazo hilo linatolewa siku mbili tu, baada ya Saudi Arabia kutambulisha taratibu za vizuizi vipya vya safari, kwa shabaha ya kupunguza usambaaji wa virusi vya corona na baada ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO kusema mripuko huo umefikia kiwango cha janga la dunia.
Serikali ya Saudi Arabia imetoa taarifa ya maambukizi virusi vya COVID 19 kwa takribani watu 86.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )