Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 13, 2020

Wanafunzi Wa Kike Waliopanga Katika Mabweni Yasiyo Rasim hatarini Kupata Mimba

juu
SALVATORY NTANDU
Imebainishwa kuwa zaidi ya  Wanafunzi 120 waliopanga katika Mabweni yasiyorasmi (MAGETO) katika kata ya ulowa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga  wako hatarini kukatisha masomo yao kutokana na kurubuniwa na makundi ya vijana katika Jamii hali ambayo inaweza kusababisha kutomaliza Masomo kwa kupata Mimba.

Kauli hiyo imetolewa Jana na Diwani wa viti maalum (CCM) kata ya Ulowa, Gabriela Kimaro katika hafla ya Uzinduzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kata ya  Ubagwe iliyojengwa kwa nguvu za wananchi iliyoanza kupokea wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2020/21 ili  kupunguza tatizo la wanafunzi kutembea umbali wa kilomita 20 kwenda kata ya jirani ya  Ulowa.

Alisema kuwa mpaka sasa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wa kike wa kidato cha pili na cha nne  ambao wamepanga katika mabweni yasiyorasmi katika makazi ya watu (Mageto) ambayo sio rafiki huku usalama wao ukiwa ni mdogo kutokana na kukabiliwa na vishawishi vya ngono kutoka kwa wafanyabiashara ambao sio waadilifu.

“Wanafunzi wanaotoka  katika kata  ya ubagwe ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwapangishia nyumba hulazimika kutembea umbali wa kilomita 20 kila siku kwenda shule na kurudi  nyumbani jambo ambao limekuwa likisababisha wasichana wengi kutotimiza malengo yao kutokana na kukabiliwa na changamoto hiyo,alisema Kimaro.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Ulowa ,Madukwa Petro alisema kuwa kitendo cha wazazi kuwapangisha wanafunzi wao katika nyumba hizo kimekuwa kikishusha ufaulu wa wanafunzi wa kike kutokana na wengi wao kurubuniwa na wanaume hususani wafanyabiashara wa chipsi.

“Kwa mwaka 2019 jumla ya wanafunzi wa kike watatu wa kidato cha nne walipata mimba na kuacha masomo na wote walikuwa wamepanga katika nyumba hizo ambazo hazina mazingira mazuri ya kuwasaidia kujifunza,huku kwa mwaka huu kuna mwanafunzi mmoja nae amepata mimba”,alisema Petro.

Alifafanua kuwa tayari serikali imeshajenga mabweni mawili katika shule hiyo na kuimba halmashauri ya Ushetu kupeleka mwalimu wa kuangalia wasichana (Matroni) ambaye atakuwa na jukumu la kuwaangalia wanafunzi hao ili kuondokana na tatizo la mimba kwa wanafunzi hususani wanaotoka katika kata za jirani.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu,Wendere Lwakatare alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanafunzi wakike waliopanga katika mabweni yasioyorasmi wanahamia katika mabweni hayo mapya kuanzia muda wowote na kuwataka wazazi kutoa ushirikiano kwa walimu pindi wanakapoanza kuwapokea.

“Wazazi msikwamishe zoezi hili tunawaomba mchangie michango yote itakayokubalika kupitia vikao vyenu vya shule ili kuwawezesha wanafunzi wengi kuhamia katika mabweni hayo na kuondoa tatizo la wanafunzi kupanga katika makazi ambayo sio salama kwao.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa ambaye alikuwa mgeni rasm katika hafla ya ufunguzi wa shule hiyo kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof,Joyce Ndalichako alisema kuwa kufunguliwa kwa shule hiyo mpya katika kata ya Ubagwe itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya Ulowa.

Alisema kuwa serikali imedhamiria kuboresha sekta ya elimu kwa kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili wanafunzi ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa madarasa yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi na kutoa rai kwa jamii kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi hususani wakike.

Mwisho.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )