Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 13, 2020

Waziri Wa Kilimo Aiagiza Tume Ya Taifa Ya Umwagiliaji Kuanisiha Na Kutoa Takwimu Sahihi Za Eneo La Umwagiliaji Nchini

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imeiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuanisha eneo halisi la umwagiliaji na kulifanyia upya uhakiki ili serikali iwe na Takwimu sahihi za eneo la umwagiliaji nchini.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa agizo jana Tarehe 12 Machi 2020 wakati akizindua Baraza la wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo ya TANAPA Jijini Dodoma.

Pamoja na agizo hilo kadhalika, Waziri Hasunga ameagiza kuwa kila Afisa Umwagiliaji wa Mkoa na Wilaya awe na orodha ya miradi inayofanya vizuri, na isiyofanya vizuri na ukubwa wa eneo linalofaa kwa umwagiliaji katika Mkoa au Wilaya anayoisimamia.

Pia ameaiagiza Tume hiyo kuweka  utaratibu wa kuandika maandiko ya miradi angalau mawili kila Mwezi kwa ajili ya kutafuta rasilimali fedha kwa wawekezaji wa kutoka ndani na nje ya nchi.

Katika Hotuba yake Waziri Hasunga ameutaja Ujenzi wa mabwawa kuwa ni lazima uwe kipaumbele katika miradi mipya ambayo Tume inatarajia kuianzisha pamoja na kuainisha Taarifa  ya Mabwawa mangapi Tume imepanga kuyajenga.

Katika hatua nyingine Mhe Hasunga amewakanya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuacha haraka majungu badala yake kutilia msisitizo katika utendaji kazi.

Kadhalika, amesema kuwa Baraza hilo limehudhuriwa na Wakuu wote wa Idara, Vitengo, Watumishi kutoka ofisi za Umwagiliaji Mikoa na wajumbe wa TUGHE Taifa, Wajumbe kutoka Ofisi za Umwagiliaji za Mikoa, na mjumbe mmoja mmoja mwakilishi wa Wafanyakazi kutoka kila Idara, Vitengo na Ofisi za Mikoa hiyo ni  ishara ya wazi kuwa mkutano huo umekidhi matakwa ya Sheria ya Majadiliano katika Utumishi wa Umma Na. 19 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2005 pamoja na Mkataba wa makubaliano ambao umeafikiwa na pande zote mbili ambazo ni Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji  na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Tanzania (TUGHE).

Amelitaja Baraza la Wafanyakazi kuwa ni chombo muhimu sana ambacho kimepewa nguvu kisheria ili kuwapa watumishi nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya masuala mbalimbali yanayohusu utendaji na ufanisi wa Taasisi ili kuongeza tija mahali pa kazi.

MWISHO
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )