Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, April 1, 2020

Halima Mdee Akwama Kufika Mahakamani Kisa Maumivu ya Mkono, Kesi Yapigwa Kalenda

juu
Mdhamini wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mshtakiwa huyo ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana ana maumivu makali katika mkono wake uliovunjika.
 
Mdee anakabiliwa na shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli na alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 10, 2017.
 
Mdhamini huyo amesema hayo baada ya Wakili wa Serikali, Silyvia Mitanto kueleza mahakamani leo Jumatano Aprili Mosi, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutolea uamuzi lakini mshtakiwa hayupo mahakamani hapo.
 
Kutokana na maelezo hayo Faris Lupomo ambaye ni mdhamini wake  aliieleza mahakama hiyo kuwa Mdee alikuwa anasafiri akitokea mkoani Dodoma kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria kesi hiyo pamoja na kliniki kwa ajili ya mkono wake uliovunjika.
 
"Kwa bahati mbaya akiwa safarini akitokea Dodoma kuja Dar es Salaam mkono wake umeshtuka na anasikia maumivu makali sana hivyo ameshindwa kufika mahakamani,"alieleza Lupomo.
 
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 28, 2020 kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
 
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )