Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, April 1, 2020

Kampuni Ya Japan Yasaidia Taasisi Ya Mifupa (Moi) Msaada Wa Vifaa Tiba Vya Milioni 80.9

juu
Kampuni ya EAA Co. Ltd ya nchini Japan inayojishughulisha na utengenezaji wa viungo bandia imetoa msaada wa viungo bandia vyenye thamani ya Shilingi milioni 80.9 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) leo Jijini Dar es Salaam.

Akipokea msaada huo, Mkurugenzi wa Tiba (MOI) Dkt. Samwel Swai amesema kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa matibabu ya wagonjwa wenye ulemavu wa miguu naa mikono.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya EAA Co. Ltd, Josiah Benedict amesema wameguswa na changamoto zinazowakabili watanzania ndiyo maana wameamua kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Msaada huo unatokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania Japan kwa kushirikiana na Watanzania waishio nchini Japan.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )