Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, April 1, 2020

Kesi Ya Tito Magoti na Wenzake Yapigwa Kalenda Hadi April 15

juu
Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Tito Magoti na mwenzake wamedai licha ya Serikali kupunguza msongamano mahakamani ili kuzuia uwezekano wakusambaa kwa virusi vya corona wanaishi kwa hofu kutokana na mrundikano wa mahabusu ulioko gerezani.
 
Magoti na Theodory Giyani (36) ambaye ni mtaalamu wa Tehama wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh 17 milioni.
 
Washtakiwa hao wameeleza hayo leo Jumatano mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Janeth Mtega baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Wankyo Saimon kueleza upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
 
Akieleza kwa njia ya video mshtakiwa wa kwanza Magoti alidai wamejawa na hofu sana kutokana na msongamano wa mahabusu waliopo gereza la Segerea
 
Amesema tangu kesi hiyo imeahirishwa siku 14 zilizopita hawajapata nafasi ya kuwasiliana na wakili wao kujua hali za familia ikiwemo mke, watoto na ndugu hivyo wanahisi kutengwa.
 
Wakili Wankyo amesema tangu kutangazwa kwa ugonjwa wa corona Serikali ilitangaza tahadhari mbalimbali na hakuna mtanzania yeyote aliyebaguliwa.
 
"Hakuna mtu yeyote aliyetengwa, gereza limechukua tahadhari ikiwemo kuzuia kuingia kwa wageni hivyo upo utaratibu waliojiwekea wao,"
 
Wakili wa utetezi Fulgence Masawe alidai magereza wanabebeshwa kosa lisilo lao la ucheleweshwaji wa upelelezi na ukosaji wa dhamana ndio umesababaisha washtakiwa kuwepo ndani hadi leo.
 
"Tulitegemea tungeambiwa upelelezi umekamilika na kesi imeanza kusikilizwa ombi letu upande wa mashtaka kuliondoa shauri hili mahakamani ambapo watakuwa na uwezo wa kulirudisha muda wowote,"amesema Wakili Massawe.
 
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mtega aliwataka washtakiwa hao kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona kwa kufuata miongozo iliyotolewa na kuutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi.
 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 15 mwaka huu itakapotajwa tena.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )