Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, April 14, 2020

Mabalozi wa Nchi za Afrika wakutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje China Kuzungumzia Ubaguzi Wanaofanyiwa Waafrika Huko China

juu
Mabalozi wa Nchi za Afrika wamekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje China, Chen Xiaoding kuzungumzia changamoto zinazowakabili baadhi ya raia wa Afrika katika mji wa Guangzhou

Chen amewaeleaza Mabalozi kwamba Serikali ya China haiungi mkono vitendo vya ubaguzi dhidi ya yeyote.

Kuhusu changamoto zilizowasilishwa na Mabalozi wa Nchi za Afrika zinazowakabili Waafrika nchini China, China imesema Mamlaka ya Jimbo la Guangdong itachukua hatua kuzishughulikia ikiwemo Raia wa Afrika ambao wameondolewa kwenye makazi na hoteli kupatiwa makazi mbadala ya muda.

China imewaahidi Mabalozi wa Nchi za Afrika kuwa itahakikisha zoezi la udhibiti wa corona linaendeshwa kwa usawa, kutoa elimu kwa umma ili kuepuka hatua zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni ubaguzi na Kuanzisha mtandao wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Nchi hiyo na Ofisi za Kibalozi.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )