Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, April 20, 2020

Maelfu Waandamana Israel Kumpinga waziri Mkuu Benjamin Netanyahu Anayekabiliwa na Mashitaka Ya Ufisadi

juu
Maelfu ya raia wa Israel, wakiwa wamevaa barakoa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, wameendelea kuandamana katika mji wa Tel Aviv dhidi ya waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Benjamin Netanyahu, Waziri anaye maliza muda wake anatarajiwa kuhukumiwa mwezi ujao wa Mei kuhusu madai ya ufisadi, ambayo ameendelea kukanusha.

Bw. Netanyahu anaendelea na mazungumzo na hasimu wake kutoka mrengo wa kati, Benny Gantz, kiongozi wa muungano wa chama cha mrengo wa kati, Blue and White alliance, kuhusu makubaliano ya muungano wa serikali ili kumaliza uhasama wa kisiasa unaodumu sasa mwaka mmoja, baada ya chaguzi tatu za wabunge ambazo walishindwa kupata idadi kubwa ya wajumbe katika Bunge la Israel (Knesset).

Maandamano yanaruhusiwa nchini Israeli licha ya hatua zilizochukuliwa kukabiliana na janga la Covid-19, ambapo waandamanaji wanaheshimu sheria za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Wakishikilia bendera nyeusi, waandamanaji hao walikuwa wakiimba katika maamnadamano yao ya Jumapili "Tuilinde demokrasia", huku wakitoa wito kwa Benny Gantz asifikie makubaliano na Waziri Mkuu anayeshutumiwa makosa ya ufisadi.

Gantz aliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba serikali ya baadaye itakuwa "safi" lakini tangu wakati huo, alisema kuwa mgogoro wa kiafya unamlazimisha atenguwe ahadi yake.

Zaidi ya visa 13,000 vya maambukizi na vifo 172 vinavyohusiana na ugonjwa huo vimeripotiwa nchini Israel.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )