Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, April 20, 2020

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro Aungana na waandamanaji kupinga amri ya kubaki nyumbani kisa Corona

juu
Rais Jair Bolsonaro wa Brazil ameamua kujiunga na mamia ya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi mjini Brasilia kupinga amri ya kubakia nyumbani iliyotangazwa na magavana wa majimbo nchini humo.

Kundi la waandamanaji zaidi ya 600 lilipiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi la nchi hiyo jana Jumapili April 19, 2020 likipinga amri ya kusalia majumbani ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona.

Rais Bolsonaro aliwaambia waandamanaji kuwa amejiunga pamoja nao kwa sababu anakubaliana na mawazo wanayotoa. 

Hata hivyo taifa hilo la Brazil lina idadi kubwa ya maambukizi  ya Virusi vya Corona katika eneo la Amerika ya Kusini. Waliombukizwa hadi sasa ni 38,000 huku vifo vikiwa ni 2400.

Mara kadhaa kiongozi huyo amekosoa hatua zilizochukuliwa na magavana za kuweka vizuizi vya wastani ikiwemo kwenye miji yenye idadi kubwa ya watu ya Sao Paulo na Rio de Janeiro ili kuzuia kusambaa virusi vya corona.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )