Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 3, 2020

UPDATES: Mgonjwa Mwingine Wa Corona Apona Nchini Tanzania

juu
Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema kuwa mgonjwa mwingine aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini amepona.

Waziri Ummy amesema hayo leo Ijumaa Aprili 03, 2020 katika taarifa aliyoitoa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii ikiwemo akaunti ya Twitter ana Instagram.


Amesema kuwa mgonjwa mmoja aliyekuwa Ngara mkoani Kagera amepona na kufikisha idadi ya waliopona corona kuwa watatu.


“Mungu ni mwema. Na leo pia hatuna case mpya za COVID19. Mgonjwa wa Kagera (Ngara) amepona. Sasa jumla ya waliopona ni 3” ameandika waziri Ummy


“Mgonjwa aliebaki wa Arusha vipimo vyake siku ya 9 leo ni Negative. Tutampima siku ya 14 ili kujiridhisha kama amepona. Wagonjwa wengine 15 waliobaki wanaendelea vizuri,” amesema.


Waziri huyo ametoa rai kwa wananchi kuepuka misongamano na mikusanyiko na kufuata maelekezo ya wataalam ili kujikinga na maambukizi hayo


chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )