Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, May 24, 2020

China Yakaribisha Juhudi za Kutambua Chanzo cha Virusi Vya Corona Lakini Kwa Masharti

juu
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema taifa hilo liko wazi kushirikiana na jamii ya Kimataifa ili kutambua chanzo cha mripuko wa virusi vya corona lakini ametahadharisha kuwa uchunguzi ufanyike bila kuingiliwa kati kisiasa. 

Wangi Yi ameifokea Marekani kwa kile alichokiita kama juhudi za wanasiasa wa taifa hilo kueneza uvumi kuhusu chanzo cha mripuko huo na kutaka kuinyanyapaa China. 

Marekani na Australia katika wiki za hivi karibuni zimetaka kufanyika uchunguzi kamili juu ya chimbuko hasa la virusi hivyo. 

Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na Waziri wake wa mambo ya kigeni Mike Pompeo wameishutumu China kwa kutokuwa wazi kuhusiana na virusi hivyo, na mara kadhaa wamerejelea semi zao kwamba virusi hivyo vimetoka katika maabara ya China.

-DW
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )