Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, May 10, 2020

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Wapungua Hadi Asilimia 3.3 % Kutoka Asilimia 3.4%.

juu
Mfumuko wa  bei wa Taifa  kwa mwaka ulioishia  Mwezi April,2020 umepungua  hadi asilimia 3.3 %kutoka asilimia 3.4% kwa mwakaulioishia Machi 2020.

Hayo yamesemwa juzi jijini Dodoma  na   Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na takwimu za Jamii Bi Ruth Minja     wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa hii inamaanisha kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei  za bidhaa na huduma kwa mwakaulioishia  mwezi April ,2020 imepungua  ikilinganishwa na kasi  iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mwezi Machi ,2020.
 
Kupungua kwa mfumuko wa bei ulioishia kwa mwaka ulioishia  April,2020 kumechangiwa kupungua kwa  bei za baadhi ya bidhaa za vyakula  na bidhaa zisizo za vyakula  kwa kipindi kilichoishia n Mwezi April ,2020 ikilinganishwa na bidhaa za mwezi April,2019.
 
Aidha,Bi Minja ameainisha baadhi ya bidhaa  za vyakula zilizopungua bei  kwa mwezi April,2020  ikilinganishwa na mwezi April,2019 kuwa ni pamoja na unga wa ngano  kwa asilimia 1.4%,matunda kwa asilimia 6.8%,viazi vitamu kwa asilimia 5.5%,na ndizi za kupika kwa asilimia 7.9%.
 
Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula  zilizopungua bei kwa mwezi April,2020 ikilinganishwa na bei za Mwezi April,2019  ni pamoja na mafuta ya taa  kwa asilimia 4.6%,dizeli kwa asilimia 7.2%  na petrol kwa asilimia 3.8%.
 
Pia Bi.Minja ameainisha baadhi ya vyakula na vinywaji baridi  kwa mwaka ulioishia mwezi April 2020 u umepungua hadi asilimia 4.6% kutoka asilimia 5.3%kwa mwaka ulioishia mwaka ulioishia mwezi  kwa mwaka ulioishia mwezi Machi ,2020.

Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ,nchini Kenya mfumuko  wa bei  kwa mwaka ulioishia Mwaka ulioishia mwezi April 2020 umeongezeka hadi asilimia 5.62% kutoka asilimia 5.51% kwa mwaka ulioishia Mwezi Machi,2020 na nchini Uganda umeongezeka asilimia3.2% kutoka  asilimia 3.0%.
 
MWISHO.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )