Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, May 19, 2020

RC Makonda Awataka Waliofunga Baa, Mahoteli Kisa Corona Wafungue Wachape Kazi.....Walikimbilia Mikoani Pia Warudi

juu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Watu wote waliofunga Hotel, Migahawa na sehemu za biashara kutokana na hofu ya Corona kuzifungua na kuanza kazi kama kawaida huku akiwataka waendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya.

RC Makonda ametoa wito pia kwa Wale waliokimbilia mikoani kwa kuhofia Corona kuhakikisha wanarudi na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

Aidha RC Makonda ametangaza siku ya Jumapili ya wiki hii kuwa siku ya Sherehe na Shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Janga la Corona ambapo ameeleza kuwa atafurahi kuona kila mmoja anasherekea siku hiyo.

“Rais Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa Makuu aliyotutendea.

"Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya kwenye ukuta wa Yerico, kwahiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida” Amesema RC Makonda
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )