Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, May 29, 2020

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Sita (06)

juu
Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188


ILIPOISHIA
“Nina waamini sana, tena hakuna ambaye ana weza kuenenda kinyume na mimi. Unacho paswa ni wewe kunipatia milioni arobaini za kuwalipa tu”
“Usijali pesa sio tatizo kwangu, jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba wana mshikilia hadi wiki ijayo, na akiondoka kuelekea nchini Nigeria, yule kimada wake aliye panga kumnunulia nyumba na kumfungulia mgahawa nitamuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.”
Maneno hayo ya Mrs Sanga yakamfanya Magreth kuhisi haja ndogo ikianza kumtoka. Kama mwana mama huyo amefanya maamuzi ya kumteka mume wake bila ya huruma na yeye ndio anaye fwatia kuuwawa, je itakuwaje endapo wata muona nyuma ya sofa hilo.

ENDELEA
Magreth cha kwanza alicho weza kukiwazia, ni kuzima mlio katika simu yake kwa maana hajui muda wala saa, watekaji wanaweza kumpigia. Wazo la kurekodi kwa siri kila kinacho endela ndani ya chumba hicho likamjia kichwani mwake. Akaweka upande wa video katika simu yake na kuanza kuwarekodi mrs Sanga na Tomas.
“Sawa, ila kwa nini usiwape hao vijana kazi ya kumuua Magreth?”
Swali hilo la Tomas, likamfanya Magreth kuushika mdomo wake na kuzidi kushangaa jinsi watu hao ambao  nyuso zao zinaonyesha ni wema, kumbe ni chui walio jivisha ngozi za kondoo.
“Etiii ehee?”
“Ndio mpenzi wangu na nina imani wana weza kumpoteza akapotea kabisa na hakuna atakaye jua kama sisi ndio tumehusika”
“Sawa tuachane na hayo baby, nipe vitu vitamu vitamu”
Mrs Sanga alizungumza huku akivua gauni lake. Magreth akaendelea kurekodi kila jambo kwa umakini sana huku akishangazwa na tabia chafu ya mrs Sanga ambaye ana heshimika sana ndani ya kanisa la mume wake.

“Hizo milioni arubaini inabidi nikakutolee bank leo”
“Nitashukuru sana mke wangu”
“Ila hakikisha una waambia hao watekaji kwamba wasimdhuru kwa kumpiga”
“Nimesha waeleza hilo jambo”
“Pia waeleze wampatie chakula anacho hitaji”
“Usijali”
“Sawa tuwahi kupita bank, nikatoe pesa hiyo kisha uwapelekee”
Mrs Sanga na Tomas wakapeana denda zito kisha wakaliweka sawa sofa walilo litumia kufanya dhambi ya kuzini.     Wakatoka ofisini humo na kuelekea lilipo gari, kwa jinsi Tomas alivyo ingia akiwa amejificha kwenye siti za nyuma za gari la Mrs Sanga ndivyo jinsi alivyo jificha kipindi Mrs Sanga anatoka getini kwa mlinzi. Hii yote ni kuhakikisha kwamba mlinzi hagundui chochote. Magreth akatoka nyuma ya sofa hilo huku akiwa haamini kwa kile alicho kiona na kukisikia. Ili kudhibitisha kwamba haoti wala hayupo kwenye ulimwengu wa kufikirika. Akarudia kuitazama video hiyo ya ngono, inayo muhusisha mrs Sanga na Tomas.
“Mungu nisaidie”
Magreth akafungua mlango kwa umakini, akachungulia nje. Alipo hakikisha hakuna mtu akatoka huku akijiweka sawa nguo zake. Akaingia kanisanani na kutokea kwenye mlango mkubwa wa kanisa, ili mlinzi asielewe chochote.
“Mage, umeonana na mama mchungaji?”
Mlinzi alimuuliza huku akimtazama usoni mwake.
“Hapana sijaonana naye”
“Ametoka sasa hivi. Basi atakuwa alifikia ofisini kwa mume wake.”
“Amesemaje kuhusiana na kupatikana kwa nabii?”
“Amenisalimia tu na hajaniambia chochote”
“Sawa kaka acha mimi nielekee nyumbani”
“Haya Magreth, tuendelee kumuombea nabii kwa maana, akipata matatizo makubwa yatakayo pelekea kufa, basi sisi wengine kazi zetu tutazisikia kwenye bomba”
“Usijali, Mungu ni mwema. Atasikia maombi yetu”
“Haya bwana”
Magreth akatoka getini hapo huku akiwa haamini kwamba amefanikiwa kutoka na kiasi hicho cha pesa. Ujasiri ukatawala moyoni mwake. Hakuwa na mashaka kutembea na kiasi hicho cha pesa alicho kibeba mgongoni mwake.
    Akapanda pikipiki na moja kwa moja akaeleka hadi nyumbani kwake. Akaliweka begi hilo kitandani, akafungua na kutazama pesa hizo za kigeni ambazo leo hii ndio mara yake ya kwanza kuzishika. Akaitafuta namba ya watekaji, akaipiga. Simu ikaita kwa sekunde ishirini na kupokelewa.
“Pesa ninazo”
Magreth alizungumza kwa kujiamini sana.
“Una usafiri?”
“Hapana”
“Ngoja tutakupigia”
Simu ikakatwa na kumfanya Magreth kubaki na mshangao. Akavua gauni alilo livaa, akatafuta suruali ya jinzi na kuivaa. Akavaa tisheti pamoja na raba, akachukua kofia ya chama  na kuivaa. Akaiweka simu yake sauti ili hata watekaji watakapo mpigia basi aweze kuisikia simu hiyo. Dakika kumi hazikuweza kuisha, akapokea simu kutoka kwa watekaji na kuanza kupatiwa maelekezo ya nini afanye.
                                ***
Mrs Sanga na Tomas wakafika katika benk ya Bacrayse.
“Baki hapa, na usionekane kwenye gari endelea kuilaza siti yako hivyo hivyo”
“Sawa mke wangu”
Mrs Sanga akambusu Tomas mdomoni mwake. Akavaa miwani yake vizuri na kujifunika mtandio ili isiwe jambo rahisi kwa watu kuweza kumfahamu kwa maana na yeye ni maarufu kama mume wake. Akaanza kutembea kwa mwendo wa umakini hadi ndani ya benki. Moja kwa moja akaelekea mapokezi.
“Habari dada”
“Salama tu”
“Nahitaji kutoa pesa, ila nina hitaji kuonana na meneja”
“Sawa, naomba nifwate”
Mwana dada huyo aliye valia sketi fupi nyeusi pamoja na tisheti ya bluu bahari, akaanza kutembea hadi katika ofisi ya meneja wa tawi hilo.
“Habari yako baba”
“Salama tu karibu sana mrs Sanga”
Meneja alizungumza huku akimtazama Mrs Sanga usoni mwake. Imekuwa ni rahisi sana kwa meneja huyo kuweza kumfahamu mrs Sanga kwa maana na yeye ni miongoni mwa waumini wa kanisa la mume wake.
“Nashukuru”
“Kwanza nichukue nafasi ya kukupa pole kwa kila lililo tokea. Mungu akapate kumsimamia nabii wetu na aweze kurudi akiwa salama salmini”
“Amen. Ni mapito kwenye dunia ila Mungu ni mwema. Nimekuja hapa kwa ajili ya kutoa milioni arobaini. Nisinge penda watu waweze kufahamu kama nipo ndani ya benki hii”
“Sawa mama, ila ninaweza kufahamu unazitoa kwa ajili ya kufanyia kazi gani?”
Swali la meneja likamfanya mrs Sanga kukaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akitafakari nini cha kumjibu meneja.
“Ni kwa matumizi yangu binafsi”
“Natambua ni hali gani ambayo una ipitia kwa sasa mrs Sanga. Ila kama ni pesa ya kuwalipa watekaji kwa ili wamuachie mume wako. Ni vyema ukanipa nafasi ya kukushauri.”
Meneja alizungumza kwa upole huku akiendelea kumtazama mrs Sanga.
“Ninaimani watakuwa wamekuagiza hicho kiasi cha pesa. Ila ningependa ushirikiane na polisi ili muweze kuweka mtego wa kuwakamata hao watekaji. Utakuwa ume muokoa nabii pamoja na pesa wanazo hitaji kupatiwa”
“Nitaufanyia kazi ushauri wako. Ila tafadhali unaweza kunipatia hizo pesa?”
“Ndio, jaza fomu hiyo hapo kisha nitalishuhudilikia hili jambo”
“Nashukuru”
Mrs Sanga akaanza kujaza fomu ya kutoa pesa aliyo pewa na meneja huyo. Alipo hakikisha kwamba amemaliza kuijaza na kusaini. Akamkabidhi meneja fomu hiyo.
“Naomba unisubirie hapa”
Meneja alizungumza na kutoka ofisini hapo na kuelekea kwa muhasimu wa benki hiyo. Ila akiwa njiani akapata wazo ambalo kwa namna moja akaamini kwamba linaweza kumsaidia mrs Sanga. Akatoa simu yake mfukoni na kuitafuta namba ya mkuu wa polisi wa kanda maalumu.
“Habari bwana Chacha”
“Salama mzee Albet, ni siku nyingi hatujawasiliana?”
“Ni kweli mambo nimengi sana si unajua mambo ya kibenki”
“Ni kweli”
“Hivi mumefikia wapi katika swala la kumpata nabii Sanga?”
“Mmm!! Bado tunaendelea kufanya upelelezi kwa umakini sana.”
“Sasa nina imani kwamba nimepata mtu ambaye ana weza kuwasaidia kumpata nabii Sanga sehemu aliyo tekwa”
“Ni nani tena huyo!!?”
“Mke wake yupo hapa benki kwangu, amekuja kutoa kiasi cha milioni arobaini, nina imani kwamba watekaji watakuwa wamempigia na kumpa vitisho vya kutoa kiasi hicho cha pesa ili awapatiea. Nina imani muna utaalamu wa kuhakikisha kwamba muna mfaatilia na kujua ni wapi na nani atamkabidhi hizo pesa”
“Nashukuru sana mzee Albet. Nitatuma vijana waanze kumpeleleza, unacho paswa kufanya ni kuhakikisha kwamba una mchelewesha hadi vijana wangu kufika hapo benki”
“Sawa Chacha”
“Nashukuru sana kwa taarifa hii muhimu kwetu.”
“Sawa”
Meneja kakata simu na kuelekea kwa muhasibu. Akamkabidhi fomu hiyo aliyo ijaza mrs Sanga, na wakadhibitisha juu ya utolewaji wa pesa hiyo. Kisha pesa hizo zikaanza kuhesabiwa, zilipo fika milioni arobaini zikafungwa vizuri na kuingizwa kwenye mfuko maalumu wenye nembo za benki hiyo . Meneja akarudi ofisini kwake.
“Samahani sana kwa kuchelewa kidogo mtandao ulikuwa una sumbua.”
“Usijali mzee wangu”
“Pesa zote zipo hapa, milioni arobaini”
“Asante na ubaki salama”
Mrs Sanga alizungumza huku akichukua pesa hizo, wakapeana mkono na meneja kisha akatoka. Kabla hata meneja ajampigia simu kamanda Chacha, simu yake ikaita.
“Ndio kamanda”
“Vijana wangu wamesha fika hapo wamevaa nguo za kiraia. Mama Sanga amevaaje?”
“Amevaa gauni jeusi, miwani nyeusi na emejifunika mtandio wa rangi ya machungwa”
“Sawa”
Simu ikakatwa. Mrs Sanga, akaanza kutembea kuelekea kwenye gari lake huku akiwa ameinamisha uso wake chini, pasipo kujua kwamba tayari polisi wamesha anza kumfaatilia.
                                ***
“Mkinga!!?”
Magreth aliuliza kwa mshangao sana. Japo anaishi nchi hii ya Tanzania ila eneo hilo halifahamu na wala hajawahi  kulisikia.
“Ndio ni wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga. Hakikisha una fika hapa kabla ya saa mbili usiku”
Baada ya mtekaji huyo kutoa maelekezo hayo, akakata simu na kumfanya Magreth ashushe pumzi taratibu. Akafungua begi lake lake kubwa la nguo. Akatoa laki tano kati ya laki tisa zilizomo kwenye begi hilo, akazishindilia kwenye mfuko wa suruli yake. Akalifunga zipu begi lenye pesa na kuliva amgongoni. Akatoka ndani kwake na kuufunga mlango wake vizuri na kuondoka. Akafika katika kituo cha waendesha taksi ambao wengi wao wana mfahamu kwani ni wateja wake wazuri sana wa maandazi.
“Mage mbona siku mbili hizi huonekani?”
Dareva mmoja alimchangamkia mara baada ya kumuona.
“Yaani Shebi wee acha tu, nina matatizo”
“Matatizo gani sister?”
“Panya road walinikaba na kuchukua hadi msingi wangu wa biashara”
“Weee usiniambie”
“Ndio hivyo, yaani hapa nilipo nina matatizo makubwa sana. Hivi gari lako linaweza kwenda masafa marefu”
“Masafa marefu kama yapi, au unataka twende mkoani?”
“Yaa nahiji twende Mkinga, una pafahamu?”
“Ndio napafahamu na gari langu lina kwenda bila shaka. Tena nimetoka kuitoa gereji asubuhi ya leo, nimeibadilisha vitu vingi sana, na matairi yote hayo ni mapya, hivyo chombo kipo poa kwenye safari”
“Sawa, twende basi”
“Sasa hivi?”
“Ndio Shebi”
“Sawa tuingie kwenye gari”
Wakaingia ndani ya gari huku Shebi akiwa haamini kama Magreth anaweza kumlipa kiasi cha pesa atakacho mtajia kwa maana siku zote wana muona ni mfanya biashara mdogo mdogo.
“Kabla hatujaondoka Magreth tukubaliane kabisa bei”
“Utanipeleka kwa sh ngapi?”
“Laki mbili kwenda tu. Kama utarudi na mimi basi laki mbili”
“Kwa hiyo ni laki nne?”
“Ndio”
Magreth akazama mfukoni mwake na kutoa laki tano hiyo, akaihesabu na kumkabidhi Shebi laki nne na kumuomba waianze  safari ya kueleka Mkinga haraka iwezekanavyo.
                            ***
    Wapelelezi wawili wa jeshi la polisi, wakazidi kumfwatilia mrs Sanga jinsi anavyo ondoka na gari lake katika eneo la benki . Wakiwa na gari lao aina ya Toyota Alateza wakazidi kulifwata kwa nyuma gari la Mrs Sanga pasipo yeye mwenyewe kujua chochote.
“Hii pesa hakikisha kwamba una wapelekea leo Tomas”
Mrs Sanga alizungumza huku akimkabidhiTomas pesa hiyo.
“Sawa mke wangu.”
Tomas alijibu huku akiwa ameilaza siti ya mbele ya gari hilo, ili watu wasiweze kumuona.
“Maelekezo niliyo kupatia hakikisha kwamba huyasahau”
“Sinto yasahau mpenzi wangu”
“Nakupenda sana Tomas wangu”
“Nakupenda pia mpenzi wangu”
Tomas alizungumza huku akipandisha juu gauni la mrs Sanga

Tumefika baba yangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akisimamisha gari lake nyuma ya gari la Tomas alilo liacha kwenye maegesho ya ofisi za rafiki yake.
“Haya shuka, acha mimi niwahi nyumbani”
“Sawa mke wangu”
Tomas taratibu akafungua mlango wa gari la mrs Sanga na kushuka huku akiwa na mfuko wenye pesa. Mpelelezi mmoja akaanza kazi ya kumpiga picha Tomas bila ya yeye kufahamu. Huku mpelelezi mwengine akitoa ripoti kwa mkuu wao kwamba wamempata jambazi aliye mteka nabii Sanga.
                                                                                                   ITAENDELEA
Haya sasa Tomas ametiliwa mashaka kama mtekaji wa nabii SANGA.Je atajitoa vipi mikononi mwa polisi. Magreth naye yopo njiani akitekeleza agizo la watekaji.  Je atafanikiwa kumuokoa nabii Sanga ikiwa mkononi mwake ana ushahidi wa uchafu wa mrs Sanga na Tomas?. Nini kitatokea? Endelea kufAatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 07
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )