Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile inaeleza matakwa ya msingi ambayo yanapaswa kuzingatiwa na wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa barakoa hizo.
Matakwa hayo ni;
- Kitambaa kiwe cha pamba (cotton) kwa asilimia 100
- Kitambaa kiwe na uzito wa GSM 90-130
- Barakoa iwe na tabaka (layers) zisizopungua mbili
- Barakoa iwe na uwezo wa kuruhusu upumuaji kwa urahisi
- Iweze kuvalia na kufunika pua na mdomo vizuri
- Kitambaa kisiwe chenye kuchuja rangi (kwa kitambaa chenye rangi)
- Iweze kufuliwa na kunyooshwa kwa pasi au kuanikwa juani bila kuathiri ubora wa kitambaa
Aidha, shirika hilo limesema linaendelea na maandalizi ya viwango mbalimbali vya vifaa vya kinga binafsi (Personal Protective Equipments-PPE).
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )