Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, June 2, 2020

ACT- Wazalendo Walalamika kutozingatiwa kwa maoni ya vyama vya upinzani katika mchakakato wa mabadiliko wa maadili ya uchaguzi

juu
Chama cha ACT- Wazalendo kimelalamikia kutozingatiwa kwa maoni ya vyama vya upinzani katika mchakakato wa mabadiliko wa maadili ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza leo na vyombo vya habari katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Magomeni  jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewalazimisha kusaini maadili hayo bila kuzingatia maoni yao jambo ambalo amedai linaweza kuvuruga uchaguzi huo.

“Mojawapo ya kanuni mbovu ni ile inayosema kwamba kura zitapigwa, zitahesabiwa, matokeo yatapatikana yatajazwa kwenye fomu za matokeo, halafu nini kinafuata? kanuni hizi zinasema msimamizi wa uchaguzi anaweza kumpa wakala nakala ya matokeo kama kutakuwa na nakala za kutosha ,“ amesema Shaibu

Baadhi ya Kanuni zinazolalamikiwa katika rasimu hiyo ni pamoja na mawakala kudaiwa kunyimwa hati za viapo kwa mujibu Katibu Mkuu huyo utaratibu uliowekwa kikanuni wa wasimamizi wa uchaguzi kutuma orodha na utambulisho wa mawakala kwa wasimamizi wa vituo umeelezwa kuwa utatumika na wasimamizi wa uchaguzi wasio waadilifu kutowasilisha majina ya mawakala wa vyama vya upinzani.

Lingine ni kutoruhusiwa kwa waangalizi wa uchaguzi kuripoti katika vyombo vya habari wanapobaini mapungufu katika uchaguzi na kuwekewa masharti ya kuripoti mapungufu hayo baada ya uchaguzi kukamilika .

Malalamiko ya aina hiyo pia hivi karibuni yalitolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) John Mnyika ambaye hata hivyo alikiri kusaini maadili hayo kwa maelezo kuwa wataendelea kuzipinga ili kuepuka kukosa kushiriki uchaguzi iwapo chama cha siasa hakitasaini kanuni hizo kama iliyoelezwa katika rasimu ya kanuni hizo.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )