Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 15, 2020

Freeman Mbowe Ajitosa Kugombea Urais wa Tanzania

juu
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe  leo Juni 15, 2020, ameandika barua ya kutia nia kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.

Mbowe ametia nia hiyo leo Jumatatu tarehe 15 Juni 2020 baada ya kupelekewa barua iliyoandikwa na baadhi ya wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wa chama hicho ili aisaini na kupelekwa Ofisi ya Katibu Mkuu.

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, amepelekewa barua hiyo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, anakoendelea kupata matibabu baada ya kudaiwa kushambuliwa  usiku wa kuamkia tarehe 9 Juni 2020.


Hatua ya Mbowe kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho, kinazidisha joto la urais ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Joto hilo, linatokana na waliokwisha kujitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa na ushawishi ndani ya chama hicho hivyo kukipa wakati mgumu kumpata mmoja.

Wengine waliokwisha jitosa ni; Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Tundu Lissu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu na mwanachama wa chama hicho, Dk. Maryrose Majige.
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )