Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 13, 2020

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya 16

juu
Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA
“Kamera na sound record katika chumba hicho zote zime zimwa kwa hiyo utakacho kizungumza hapo kitaishia ndani humo. Mimi nipo hapa mlangoni nina kusubiria”
RPC alizungumza huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.


“Sawa”   
Nabii Sanga akaingia ndani ya chumba hicho na kumfanya Tomas ashtuke sana kwani hakutarajia kumuona nabii Sanga kwa wakati kama huu kwa namna moja ama nyingine alihisi kwamba Rama D na wadogo zake watakuwa wamemuua, kwani aliwashuhudia rafiki zake hao wakifa peke yao pasipo uwepo wa nabii Sanga.

ENDELEA
Nabii Sanga wala hakujali kustuka kwa Tomas, akavuta kiti huku akitazama kamera nne zilizo fungwa kwenye kila kona ya chumba humo ndani.
“Habari yako Tomas”
Nabii Sanga alianza kuzungumza huku akimtazama Tomas anaye kwepesha macho yake kutazamana na nabii Sanga, kwani ubaya wote alio utenda kwa mtu huyo umemrudia yeye mwenyewe.
“Niambie ni wapi nilikukosea?”
“Aha…ahaa baba ni…ni…sa…s…amehe”
Tomas alizungumza kwa kubabaika huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake. Nabii Sanga akatoa simu yake, na kuingia kwenye email yake na kuitazama video ya Tomas na mke wake wakifanya mapenzi ofisini kwake. Akamgeuzia Tomas video hiyo na kuzidi kumfanya Tomas awe katika wakati mgumu.
“Huyu ni mke wangu, tena mwanamke uliye kuwa una muheshimu kama mama yako wa kiroho. Leo hii una muingilia kinyume cha maumbile na yeye ana furahia sana. Niambie nikufanye nini?”
Tomas akashindwa kujibu swali hilo zaidi ya kuanza kuangua kilio, huku akitamani ardhi ipasuke na immeze.
“Nilikupa kazi zangu nyingi, nilikuamini sana Tomas, kwa nini umekuwa msaliti kwangu. Kwa nini umeamua kuharibu hatima ya familia yangu kwa nini?”
Nabii Sanga alizungumza kwa sauti ya upoe ila iliyo jaa msisitizo wa mtu ambaye amekasirishwa sana kwa kitendo hicho.
“Nashukuru kwa kila jambo Tomas.”
Nabii Sanga mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, akasimama na kutoka ndani humo
“Umemaliza mzee?”
RPC alimuuliza nabii Sanga huku akimtazama usoni mwake.
“Ndio, hakikisha hii siku ya leo haimalizi”
“Sawa nitafanya hivyo”
Wakarudi kwa pamoja ofisini kwa RPC huku nyuma wakimuacha Tomas akizidi kuugulia maumivu ya moyo wake. Akajikuta akijilamu ni kwa nini alikubali ushawishi wa mrs Sanga na kuingia naye kwenye mahusiano yake. Akazidi kujilamu ni kwa nini alikubali kupanga mpango wa kumteka nabii Sanga. Nabii Sanga akahamisha kiasi cha pesa walicho kubaliana na RPC kutoka kwenye akaunti yake na kuingia kwenye akaunti ya siri ya RPC.
“Nitahitaji kuiona maiti yake mukisha muua”
“Sawa muheshimiwa”
“Na jambo jingine, hakikisha hii ina kuwa siri. Mke wangu sihitaji aweze kuguswa na hili jambo”
“Sawa mzee. Ila nina weza kukuuliza swali”
“Uliza”
“Je ikitokea mke wako akafanya jambo jingine kubwa zaidi ya hili la kukuteka itakuwaje?”
“Nitajua jinsi ya kudili naye. Ila yeye asikuumize kichwa juu ya usalama wangu”
“Sawa sawa, nimekuelewa”
Nabii Sanga na RPC wakaagana kisha nabii Sanga akaondoka eneo hilo la polisi. Akawasiliana na Clyaton na akamfahamisha kwamba Magreth yupo bado ofisini kwake, ana furahia juu ya kupata gari hilo.
“Nina kuja sasa hivi”
“Sawa”
Nabii Sanga akakata simu na kumueleza dereva wake ni wapi ampeleke. Wakafika dukani kwa Clayton na moja kwa moja wakaingia ofisini pasipo Magreth kumuona.
“Yule kijana kule kwenye gari na Magreth ni nani?”
Nabii Sanga aliuliza huku akiwa amesimama kwenye dirisha la ofisi hiyo huku akiwatazama Magreth na Sheby wakizungumza.
“Ahaa amekuja naye”
“Yeye ndio amekuja naye?”
“Ndio vipi mbona una shangaa?”
“Ahaa…hakuna. Ehee nipatie garama za gari alilo chagua”
Clayton akampatia nabii Sanga bei ya gari hilo. Nabii Sanga mara baada ya kumaliza kulipana na Clayton kwa kupitia njia ya kuhamisha pesa kutoka benki moja kwenye benki nyingine, akaelekea eneo alipo Magreth na Sheby. Magreth kwa furaha iliyo mtawala akashindwa kujizuia na kujikuta akimkumbatia nabii Sanga kwa furaha sana.
“Asante sana baba”
Magreth alizungumza kauli hiyo ili kuficha siri ya mahusiano yao.
“Usijali mwanangu. Huyu ni nani?”
“Ni Sheby, dereva taksi aliye nileta hapa kutoka kule mtaani kwetu na kunizungusha mji mzima”
“Ahaa..kijana una mdai kiasi gani Mage?”
“Alaa laki na nusu”
Nabii Sanga akaingiza mkono mfukoni mwa suruali yake. Akatoa laki mbili na kumpatia Sheby.
“Sasa kazi yako ime kwisha. Unaweza kwenda”
Sheby akazipokea pesa hizo kwa furaha, akamuaga Magreth kisha akaondoka zake.
“Siku nyingine sihitaji uwe karibu karibu na hawa vijana sawa”
Nabii Sanga alizungumza kwa ukali kidogo.
“Sawa mume wangu”
“Nashukuru kusikia hivyo. Vipi ume lipenda hili gari?”
“Ndio nimelipenda”
“Sawa wana malizia vibali vyote kisha tuta ondoka nalo leo kuelekea huko unapo ishi”
“Haya”
Vijana wa Clayton mara baada ya kumaliza kufwatilia maswala ya usajili wa gari hilo. Wakamkabidhi detail zote bosi wao kisha Claytona akamkabidhi Magreth nyaraka zake na wakaondoka eneo hilo na nabii Sanga.
“Hili gari zuri sana”
Nabii Sanga alizungumza huku akiendesha gari hilo.
“Kweli?”
“Ndio, kikubwa ulitunze sana”
“Usijali, nitakuwa nina liendesha kwa umakini wa hali ya juu”
Wakafika nyumbani kwa Magrerth. Nabii Sanga akalisimisha gari hilo kwenye maegesho yaliyomo katika nyumba hiyo ambayo ipo sehemu iliyo tulia sana.
“Hapa ni pazuri sana, nime papenda”
“Kweli mume wangu?”
“Ndio, tena leo nitalala na wewe hapa kuzindua nyumba”
“Haaaa”
“Ndio. Ehee una lipa kiasi gani hapa?”
“Laki tano”
“Umeipenda hii nyumba?”
“Sana”
“Basi kesho wasiliana na mwenye hii nyumba na tumshawishi juu ya kuinunua”
“Kweli?”
“Ndio mke wangu”
Nabii Sanga na Magreth wakazidi kuzama kwenye penzi ambalo kwa upande wa Magreth amempendea pesa mzee huyo huku upando wake wa dhati ukiwa kwa Evans ambaye bado ana endelea kuuguza jeraha la kisu alicho chomwa. Upande wa nabii Sanga, moyo wake ume mpenda sana Magreth na yupo tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya mwanamke huyo.
                                ***
Mrs Sanga akafika Bagamoyo, akaelekea kwenye hoteli moja iliyopo pembezoni mwa bahari. Akachukua chumba kimoja na kulipia kwa siku mbili.
“Mawazo yangu yatapungua hapa”
Mrs Sanga alizungumza huku akijilaza kitandani. Akachukua simu yake na kuangalia picha za jogo ambazo walikuwa wakitumiana na Tomas kisiri siri kupitia mtandao wa whatsapp. Picha za  Tomas, zikaanza kumsisimua mrs Sanga. Taratibu akaanza kujishika makaja yake, huku akiipandisha juu sketi yake ndefu aliyo ivaa hadi alipomaliza haja zake.
Baada ya hapo akashuka kitandani hupo na kuingia bafuni, akaoga kisha akarudi chumbani. Saa ya ukutani katika chumba hicho ina muonyesha ni saa mbili usiku. Akavaa baibui lake kisha akatoka chumbani humo na kuelekea eneo la mgahawa mkubwa katika hoteli hiyo ya kitalii. Akatafuta sehemu yenye mwanga hafifu na kukaa. Akaagiza chakula anacho kihitaji pamoja na mzinga wa wyne ya dompo.
    Chakula kikaletwa na muhudumu na kuana kula taratibu na kunywa huku akitazama tazama watu waliomo ndani ya mgahawa huu.
‘Ila huyu mwanaume hawezi kunifanya jambo lolote, la sivyo siri zake zote nitazitoa hadharani’
Mrs Sanga alizungumza huku akiendelea kula.
‘Au nimtishe kutoa siri zake kama ata mdhuru Tomas?’
Mrs Sanga aliendelea kuwaza kichwani mwake huku akizidi kutafuna nyama choma aliyo nunua.
‘Ndio, kwa maana hata yeye ameshwa nisaliti na nikamsamehe’
Mrs Sanga alizungumza huku akianza kuwaza matukio ya nyuma ambayo mume wake alisha wahi kuyafanya. Siku moja nabii Sanga alipo rudi kutoka nchini Nigeria, alirudi akiwa ameongozana na kijana wa kiume mwenye miaka kumi. Mrs Sanga alimuuliza mume wake juu ya kijana huyo, akamueleza kijana huyo alikuja kukaa kwa muda nchini Tanzania, kisha baada ya hapo ata rudi nchini Nigeria.
Toka alipo kuja kijana huyo nyumbani kwao, mtindo wa nabii Sanga kuamka usiku wa manene ukaanza. Kwa siku za hapo awali mrs Sanga alihisi kwamba mume wake ana kwenda kasali katika chumba maalumu cha maombi kilichopo chini ya ardhi katika jumba lao hilo.
‘Mume wangu nahitaji haki yangu bwana’
Mrs Sanga alilalama huku akimshika shika nabii Sanga usiku huo.
‘Mke wangu muda wa mauombi una karibia. Acha nikasali kwanza kisha nitarudi’
‘Jamani mume wangu toka utoke huko nchini Nigeria, hujawahi kunipa haki yangu. Sasa ni wiki ya pili, una hisi kwamba mimi sina hamu na wewe’
‘Natambua mke wangu ila nina kuomba univumilie hadi nikamalize kuomba’
‘Sawa mume wangu’
Mrs Sanga alikubali kishingo upande. Saa nane kamili usiku, nabii Sanga kama kawaida yake akanyanyuka kitandani huku akiwa na biblia yake na kuelekea katika chumba hicho. Mrs Sanga siku hiyo hakukubali kumuacha mume wake akasali yeye mwenyewe. Akasubiri kama dakika kumi na tano zipite kisha na yeye akashuka kitandani. Akatembea kwa mwendo wa kunyata hadi eneo la chini, kilicho chumba hicho ambacho ni wana famili tu ndio wana tambua juu ya uwepo wa chumba hicho. Mrs Sanga akastuka mara baada ya kufika mlangoni mwa chumba hicho na kusikia sauti za kimahaba.
‘Kuna nini?’
Mrs Sanga alijiuliza huku akitafakari kufungua mlango wa chumba hicho. Akausukuma taratibu mlango wa chumba hicho. Mapigo ya moyo yakamstuka sana mara baada ya kuona mishumaa mingi iliyo wazunguka nabii Sanga na kijana kutoka Nigeria ikiwa inawaka. Mbaya zaidi wote wawili wapo uchi kabisa . Mrs Sanga akajikaza na kuingia ndani humo, ila kutokana na mstuko alio upata kutokana na kuona tukio hilo ukamfanya aanguke na kupoteza fahamu. Jambo ambalo lilimfanya nabii Sanga na kijana huyo kustuka sana na kusitisha kila walicho kuwa wana kifanya.
“Hei samahani mama. Simu yako ina ita”
Sauti ya muhudumu aliye simama mbele ya mrs Sanga ika mstua sana na kumtoa kwenye dibwi zima la mawazo ya maisha ya nyuma aliyo ishi na nabii Sanga.
“Ohoo Mungu wangu hata akili yangu sijui ipo wapi”
Mrs Sanga alizungumza hukua kichukua simu hiyo. Akatazama na kukuta ni namba ya mtoto wake wa mwisho ndio anaye mpigia. Akaipokea simu hiyo na kuiweka simu hiyo sikioni mwake.
“Mama mbona napiga simu zaidi ya mara sita hupokei”
Juliethi alilalama.
“Ohoo samahani mwanangu, nilikuwa kwenye maombi na simu nime iweka sinlece. Ehee niambie”
“Upo wapi?”
“Kuna mama mmoja yupo huku Pangani, nime kuja kumfanyia huduma ana umwa sana. Vipi umesha rudi kutoka chuo mwanangu?”
“Ndio mama. Kama upo Pangani kweli utaweza kurudi usiku huu peke yako?”
“Hapana mwanangu, labda kesho au kesho kutwa ndio nitarudi. Vipi baba yako yupo nyumbani?”
“Hapana hayupo nyumbani naye nimempigia simu amedai kwamba hato rudi nyumbani.”
“Yupo wapi?”
“Hajaniambia yupo wapi, ila amenieleza kuna mambo ana yashughulikia”
“Hembu kata simu nimtafute”
“Sawa mama”
Mrs Sanga akaitafuta namba ya mume wake huku akipiga fumba la wyne hiyo aliyo iagiza. Simu ya mume wake ikaita kisha ikakatwa. Akapiga tena, ikaita kisha ikakatwa. Akapiga tena mara ya tatu, ikaita kisha ikakatwa.
“Pumbavu”
Mrs Sanga alizungumza huku akihamia upande wa meseji.
“Naona unanikatia simu, upo na huyo malaya wako si ndio. Sasa ni hivi endapo Tomas atakwenda jela au kudhurika na jambo lolote. Nitatoa siri zako zote hadharani, sasa tuone kama hao waumini wako unao wafanya mandondocha wata kusujudia. BYE”
Meseji hiyo haikuchukua hata sekunde thelathini, ikarudisha majibu kwamba imemfikia nabii Sanga na ameisoma.
                                ***
Majira ya saa nne usiku, RPC akamchukua Tomas na kupitisha njia za siri zilizopo chini ya kituo hicho, pasipo askari wa aina yoyote kuweza kufahamu. Akafika eneo la mbali, njia nizi zilipo tokea, akamuingiza Tomas kwenye gari lake binafsi na si gari ya ofisi anayo tembelea nayo, huku Tomas akiwa amemfunga kitambaa cheusi ili aisweze kuona ni nani aliye mtoa wala kujua ni wapi anapo pelekwa. RPC katika kuikamilisha kazi hiyo aliyo pewa na nabii Sanga, hakuihitaji kuwa hewani ili wakuu wake wa kazi au wafanyakazi walipo chini yake, wampate hewani. Akazima simu yake na kuzidi kuendesha gari lake hilo huku akielekea katika mji wa Kibi lilipo shamba lake,akiamini eneo hilo ana weza kutekeleza agizo la kumua Tomas pasipo mtu wa aina yoyote kuweza kugundua.
“Muna nipeleka wapi?”
Tomas aliuliza huku akitawaliwa na wasiwasi mwingi sana. Ila ukimya ulimo ndani ya gari hilo na kuto kuona kwake kutokana na kufungwa macho kwa kitambaa cheusi huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa, ikamuashiria Tomas kwamba hali aliyo nayo hivi sasa sio salama kwa maisha yake.
                                ***
Meseji kutoka kwa mke wake, kukamfanya nabii Sanga kuchomoa jog wake kutoka kwa Magreth huku akiwa na wasiwasi.
“Baby vipi?”
Magreth aliuliza huku akimshangaa nabii Sanga akishuka kitandani. Nabii Sanga siku zote ana mfahamu mke wake, ni mtu ambaye ana simamia misimamo yake pale anapo amua jambo fulani kulifanya, tena awe ameliamua kihasira. Woga wa siri zake kuwa hadharani ukamfanya, ajikute akitengua mamauzi ya kuuwawa kwa Tomasa. Akaitafuta namba ya RPC na kumpigia, ili kumpa agizo la kusitisha zoezi hilo. Mapigo ya moyo yakazidi kumdunda nabii Sanga huku jasho likimwagika, mara baada ya kukuta namba ya RPC haipatikani hewani huku akitambua kwamba muda huu ndio wakati wa Tomasa kuuwawa kisiri.
                                                                                                ITAENDELEA
Haya sasa, mambo ni bampa tu bampa. MRS Sanga ameamua kumwaga ugali. RPC naye hapatikani hewani na endapo Tomas ata kufa basi siri za nabii Sanga ambazo mimi na wewe hatuzijua zitaanikwa hewani, nini kitatokea? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 17.
 
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )