Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, June 3, 2020

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Kumi na Moja (11)

juu
Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA
Magreth alijibu kwa sauti ya upole na iliyo jaa aibu kubwa sana. Hakutarajia siku hata moja kama atakuja kumkabidhi nabii Sanga mwili wake tena na bikra yake ambayo alikuwa akiitunza kwa ajili ya mwanaume atakaye muoa.“Ila nina ombi moja. Endapo atatokea mwanaume akakuchukua mara ya mimi kukubadilisha kimaisha. Haki ya Mungu, nitamuua mbele yako na utashuhudia jinsi nitakavyo ufanya ukatili huo. Kwani sinto kuwa na huruma kabisa na yeye”


Maneno ya nabii SANGA yakamstua sana Magreth, kwani moyo wake haupo kabisa kwa nabii Sanga kwani mwanaume anaye mpenda kuliko kitu chochote ni Evans ambaye yupo hospitalini akipatiwa matibabu kwa pesa za nabii Sanga.

ENDELEA
“Mage tume elewana?”
“Nimekuelewa baba”
“Usiniite baba, kuanzia hivi sasa mimi ni mume wako”
Mage akakosa cha kupinga kwani kama ni usichana wake tayari umesha tolewa na nabii Sanga. Taratibu nabii Sanga akamkumbatia Magreth kwa nyuma na kulala, kumalizia masaa hayo machache yaliyo salia kabla ya kupambazuka. Mlio mkubwa wa redio, inayo imba wimbo wa taarabu, ukawastua nabii Sanga na Magreth.
“Nani huyo?”
Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amekerwa na makelele hayo.
“Ni mama mwenye nyumba”
“Ndio ana washa mziki mkubwa kiasi hicho?”
“Ahaa sisi tumesha zoea”
“Hapana kwa kweli. Leo hii hii nahitaji uhame kama ni kutafuta nyumba basi katafute sehemu ambayo ni nzuri na tuhame. Ume nielewa?”
“Ndio mpenzi”
Magreth akajikaza sana moyoni mwake kuita jina hilo, lililo mfanya nabii Sanga kuachia tabasamu pana akionekana dhairi kwamba amefurahi kuitwa jina hilo. T
“Unaweza kunywa chai na mihogo mpenzi?”
“Mihogo ya aina gani?”
“Kukaanga?”
“Ndio nina weza. Tena nina hamu nayo”
“Basi leo acha nika kununulie. Nabandika chai haraka haraka tunywe kisha tuendelee na ratiba nyingine”
“Sawa baby”
Magreth akashuka kitandani, akajifunga tenge lake na kutoka nje. Akakutana na mama mwenye nyumba uwani akifagia.
“Shikamoo mama”
“Marahaba, jana nimesikia miguno ambayo sikuwa nina ielewa elewa ndani kwako. Vipi kwema?”
Maneno ya mama mwenye nyumba yakamstua sana Magreth aliye shika kindoo cha chooni chenye maji kiasi.
“Kwema”
Magreth alizungumza huku akielelea bafuni.
“Naona hata kamwendo kame badilika, ni nani huyo aliye pata bahati ya kuzibua mgodi huo wa dhahabu?”
Magreth hakuyajali maneno hayo ya karaha zaidi ya kuingia chooni. Akamaliza huduma ya haja ndogo na kuoga haraka haraka kisha akarudi chumbani kwake.
“Huyo mama anaye washa mziki mkubwa hivyo, ana mume?”
“Hana”
“Ndio maana. Ametufanya tuamke kwa makelele yake. Ila usijali haya yote yatakwisha sawa mpenzi wangu”
“Sawa baby”
Meneno ya Magreth yakazidi kumpagawisha nabii Sanga. Magreth akajiandaa na kuelekea mtaa wa pili ambao una wafanya biashara wengi wanao pika mihogo ya kukaanga pamoja na chapati. Akanunua mihogo ya kukaanga na kurejea nyumbani kwake. Akaandaa chai na kwa pamoja wakaanza kunywa na Magreth huku furaha ikiwa ime tawala kati yao.
“Muhasibu wako una muamini?”
“Yaa nina muamini sana”
“Yasije kuwa mambo ya Tomas”
“Ila ni kweli yasije kuwa mambo ya Tomas. Nitajitahidi kumuamini”
Mara bara baada ya kupata chai hiyo ya nguvu. Nabii Sanga akatumia simu ya Magreth kuwasiliana na muhasibu wake aitwaye Judithi Kiria. Akamuelekeza Judithi ni wapi alipo na akamuomba asiweze kuja na gari lake, bali atumie usafiri wa bajaji ili isiwe rahisi kwa watu wana mfahamu muhasibu huyo kumfaatilia. Ndani ya dakika ishirini Judithi Kiria akafika katika nyumba hiyo kwa msaada wa maelekezo aliyo patiwa na Magreth. Akapokelewa kwa furaha na Magreth, kwani ni watu wanao fahamiana.
“Shikamoo baba”
“Marahaba Judithi mwanangu”
“Pole sana kwa matatizo baba”
“Nashukuru mwanangu. Laiti ingekuwa si Magreth kujitoa sadaka maisha yake basi nisinge weza kuwa hapa hadi muda huu.”
“Ehee ilikuwaje kuwaje?”
Nabii Sanga akamueleza Judithi Kiria kila jambo lililo tokea hadi kufika usiku katika nyumba hiyo.
“Ohoo MUNGU ashukuriwe hawakuweza kukudhuru”
“Amen. Sasa nenda na Mage benki ya CRDB. Msaidie kufungua akaunti na ufanye uhamisho wa milioni mia mbili”
Magreth bado kidogo moyo wake umlipuke kwa shangwe, ila akajikaza kuizuia furaha hiyo.
“Kwa maana maisha yangu yeye ndio alikuwa muamuzi wa mwisho. Laiti kama angekataa kuja kule msituni basi nisinge kuwa hai sasa hivi”
Nabii alitoa sababu ya kusaidiwa, ila ukweli ni kwamba moyo wake wote upo kwa Magreth.
“Sawa baba, nitafanya hivyo”
“Jambo jengine, wewe si una ishi kule Kigamboni?”
“Ndio baba”
“Kuna nyumba nzuri nzuri za kununua au kupanga?”
“Zipo nyingi sana”
“Basi nitafutie nyumba ya kupanga. Hembu tazama maisha ya huyu binti jinsi yalipo. Sikia hayo makelele ya taarabu, japo nimelala hapa, ila sijajisikia vizuri kwa makelele hayo”
“Sawa baba ila kwa nini tusimtumie Tomas katika kutafuta nyumba nzuri kwa maana yeye ana fahamiana na watu wengi”
“Achana na Tomas”
“Naweza kujua kwa nini baba?”
Swali la Judithi Kiria likamfanya Magreth kumtazama nabii Sanga, anaye onekana kutafakari juu ya kulijibu swali hilo.
“Tomas yeye ndio alipanga mpango wa kuniteka”
“Nini?”
“Yaa alifanya hivyo kwa maslahi yake binafsi. Ila nina shukuru Mungu nilifanikiwa kutoka katika mikono ya watekaji hao mara baada ya kuwapa kiasi hicho cha pesa alicho kileta Magreth kule porini”
“Ohoo Mungu wangu!!”
“Mbona ume stuka sana?”
“Ahaa…hapana baba. Sikutarajia kama Tomas yule ninaye mjua mimi ana weza kuwa na akili za kijinga kama hizo”
“Ndio hivyo amefanya kwa ajili ya maslahi yake binafsi. Sina jinsi zaidi ya kujitenga mbali naye”
“Sawa baba nimekuelewa, acha sisi tuondoke”
Judith na Magreth wakaondoka, huku wakipita katika ofisi ya mtendaji wa eneo hilo kwa ajili ya kuandikiwa barua ambayo wataitumia benki. Wakapita eneo la kupiga picha ndogo(passport size). Walipo hakikisha wana kila kitu ambacho benki ina hitaji. Wakelekea katika benki hiyo. Kufahamika kwa Judithi Kiria, kuka rahisisha zoezi la Magreth kufungua akaunti ya benki kwenda haraka haraka.
“Una bahati sana kwenye maisha yako Magreth”
“Kwa nini?”
“Huyu mzee ni mchumi sana. Sijui imekuwaje hadi amekupatia kiasi hichi kikubwa cha pesa”
“Sijajua kwa kweli. Hivi una muda gani ume fanya kazi na baba?”
“Huu ni mwaka wa saba. Nilipo toka tu chuoni aliweza kuniajiri, nimekuwa muaminifu sana kwake, nina mshukuru Mungu hadi sasa hivi nina maisha yangu mazuri sana ambayo yana nifanya nisaidie ndugu zangu na jamaa zangu pia.”
“Hivi ana penda nini baba?”
“Hapendi mtu ambaye si muaminifu. Yaani hapa namuwazia Tomas sijui ata mfanya nini? Hapendi mtu muongo, kama una matatizo au tatizo, hakikisha una mueleza mapema kabla ya yeye kufahamu tatizo lako. Hapendi mtu asiye jibidiisha, ana chukia sana uvivu na upuuzi”
“Ahaa”
“Yaa”
“Judithi akaunti yenu ipo tayari”
Muhudumu wa benki hiyo limueleza Judithi na Magreth walio kaa kwenye eneo la kusubiria. Wakanyanyuka na kumfwata muhudumu huyo. Judithi akafwata hatua zote za kuhamisha pesa kutoka akaunti ya biashara ya kanisa la nabii Sanga kwenda akaunti ya Magreth. Magreth akaonyeshwa salio lililopo kwenye akauti yake, akatamani kuzimia kwa furaha.
“Mama umesha kuwa milionea”
Meneja wa benki hiyo alizungumza huku akijawa na tabasamu pana usoni mwake.
“Ohoo asante Mungu”
Magreth alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Akakabidhiwa kadi yakae ya kutolea pesa, akafundishwa jinsi ya kutoa pesa. Ili kudhibitisha kwamba ana pesa kwenye akaunti yake, Magreth akatoa milioni moja na ujumbe mfupi wa meseji ukaingia kwenye simu yake.
“Kwa hiyo nikitoa pesa huku muna nitumia ujumbe kwenye simu yangu?”
“Ndio dada, huduma ya ATM ime unganishwa na simu yako ya mkononi.”
Muhudumu huyo aliye mfundisha jinsi ya kutumia ATM mashine alimjibu kiufahasa.
“Pia kwa kupitia simu yako una weza kutoa na kuweka pesa kwenye akaunti yako. Hauna haja sasa ya kuja hapa benki na kupanga foleni”
Magreth akamaliza kupewa maelezo hayo. Wakaondoka benki hapo na kueleka hadi eneo Magreth alipo acha gari lake. Wakaelekea Kigamboni na kumtafuta dalali ambaye ni maarufu sana katika mji huo. Wakafanikiwa kumpata dalali, wakampa jukumu la kumtafutia Magreth nyumba nzuri ya kupangisha. Haikuwa kazi kubwa kwa maana kwa dunia ya sasa kila kitu kinapatikana kwenye mtandao. Wakaonyeshwa nyumba ambazo zipo wazi kupitia mtandao.
“Hii ina vyumba vitu ni nzuri sana”
Magreth alizungumza huku akitazama picha za nyumba hiyo.
“Basi kodi ya mwezi ni laki tano”
“Twende tukaione”
Judithi Kiria alizungu. Wakaelekea katika eneo ilipo nyumba hiyo. Katika mtaa huo kuna majumba makubwa ya kifahari na mazuri. Magreth na Judith wakatembezwa kwenye nyumba hiyo. Walipo ridika, Magreth akalipa kodi ya mwaka mzima, akaandikishana mkataba na mwenye nyumba kisha akakabidhiwa funguo. Wakarudi nyumbani kwa Magreth, wakamueleza nabii Sanga kila jambo walilo lifanya.
“Nashukuru Judithi, kaendelee na kazi na usimueleze mtu aliye yoyote juu ya hii siku wala uwepo wangu hapa”
“Sawa baba, naamimi una nifahamu na sinto weza kufanya hivyo”
“Nashukuru”
Judithi Kiria akaondoka na kumuacha nabii Sanga na Magreth. Magreth akafunga mlango wa chumba chake kisha taratibu akaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine jambo lililo mfanya nabii Sanga naye aanze kuvua nguo zake kujiandaa kwenda kushiriki na Magreth.
                                ***
“Tuna waambia nini familia yake na wana nchi?”
Mkuu wa polisi aliwauliza vijana wake walio kuwa wamekwenda kuifanya oparesheni ya kumuokoa nabii Sanga, katika kikao hicho cha dharura, katika makao makuu ya polisi.
“Inabidi tusitoe ripoti yoyote mkuu zaidi ya kuendelea na upelelezi, nina imani kwamba hawaja muua nabii Sanga kwa maana kila eneo la msitu hakuna sehemu ambayo tumekuta damu wala shimo alilo fukiwa mtu.
“Maiti za majambazi zipo wapi kwa sasa?”
“Muhimbili”
“Yule mshenzi yupo wapi?”
“Yupo mahabusu ya kwake peke yake”
“Sawa, pesa na silaha na magari walio kuwa wakitumia majambazi. Viandaeni ili niweze kuzungumza na waandishi wa habari. Hilo swala la nabii Sanga, tutaendelea kulifanyia uchunguzi wa kujua ni wapi alipo”
“Sawa mkuu”
“Tawanyikeni”
RPC alizungumza na vijana wake wakatawanyika. Mkutano wa RPC na waandishi wa habari ukaanza. Vibunda vya pesa za kigeni na pesa za Tanzania walizo kamatwa nazo majambazi, zikawekwa mezani. Silaza zao nazo zikawekwa mezani na waandishi wa habari wakaanza kuvipiga picha.
“Mapambano ya jana usiku na majambazi walio mshikilia nabii Sanga yalikuwa ni makali sana. Vijana wangu waliweza kuifanya kazi ya kuhakikisha wana kabiliana na majambazi hao na walifanikiwa kuwaua majambazi wanne. Hizi ni pesa ambazo tuliwakuta nazo, magari yao walio kuwa wana yatumia yapo hapo nje, tutawaonyesha mara baada ya kikao hichi.  Nikaribishe maswali wawili tu”
RPC alizungumza kwa kifupi na kumchagua mmoja wa waandishi habari aulize swali lake.
“Je mumefanikiwa kumpata nabii Sanga? Kama mume mpata je yupo wapi kwa sasa?”
“Kutokana na sababu za kiusalama sinto weza kukujibu maswali yako. Nakaribisha swali la pili”
“Maiti za majambazi hao kwa sasa zipo wapi?”
“Muhimbili, ila tuna endelea kuzifanyia uchunguzi ili kuweza kubainisha wao ni kina nani na tutahakikisha tuna pata muunganiko wa wao na watu walio kuwa wana wauzia silaha za kivita kama hizo AK47 munazo ziona hapo mezani. Karibuni mukayaone magari yao”
RPC akatoka ukumbini humo na waandishi wa habari wakimfwata nyuma. Akawaonyesha magari walio kuwa wana yatumia Rama D na wadogo zake. Kila aliye yaona alishangaa, kwani yamejaa matundu mengi sana yatokanayo na risasi huku moja likiwa lime bondeka bondeka vibaya sana.
                                ***
    Mrs Sanga hakuweza hata kutia kitu chochote mdomoni mwake, hii yote ni kutokana na woga ulio mjaa. Hakutarajia kumuona Tomas akiingia katika kipindi hicho kigumu. Kila aina ya maombi, ameomba kwa ajili ya Tomas, wala hakuwa na shaka na mume wake ambaye hana hata chembe ya upendo juu yake. Taarifa ya askari anayo iona kwenye luninga yake kuhusiana na majambazi walio mteka mume wake, ikazidi kumpa wakati mgumu mrs Sanga. Habari ya kuuwawa kwa majambazi hao, ikamfanya ahisi Tomas ni miongoni mwao.
“Gari lake pale halipo”
Mrs Sanga alijifariji kwa hilo.
“Mama”
Julieth aligonga mlangoni mwa mama yake, mara baada ya kuto muona akishuka sebleni toka asubuhi.
“Mmmmm”
“Fungua basi mlango”
Mrs Sanga akajifunga tenge na kumfungulia mwanaye huyo wa mwisho mlango.
“Shikamoo”
“Marahaba. Vipi mbona haujaenda chuo?”
“Nitaendaje, ikiwa maaskari wamenizuia kwenda. Vipi na wewe mbona huja toka chumbani hadi sasa hivi ina kwenda saa saba mchana?”
“Nipo kwenye mfungo wa maombi. Nina muombea baba yako huko alipo asiweze kukubwa na jambo lolote baya”
Mrs Sanga alimuongopea mwanaye.
“Sawa, ila Mungu ata simama nasi, ata kuwa salama”
“Amen”
“Ngoja nikuache uendele na maombi yako mama”
“Sawa mwanangu”
Julieth akatoka ndani humo na kumuacha mama yake akiangua kilio huku akizidi kumuomba Mungu afanye muujiza kwa Tomas ili aweze kutoka mikononi mwa askari.
                                ***
RPC mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari. Akaagiza Tomas kuingizwa kwenye gari lake, askari wake wakatii amri hiyo.
“Niacheni naye huyu kijana. Nina elekea naye Muhimbili”
“Mkuu ina bidi niongozane nawe”
Bodygard wake alizungumza kwani ni jukumu la kuongozana na bosi wake kila sehemu anayo kwenda.
“Wewe leo baki hapa. Niacheni kuna jambo nahitaji kwenda kumuonyesha”
RPC akaingia kwenye gari lake hilo aina ya Toyota VX V8 na kuondoka. Wakafika hospitali ya taifa Muhimbili. Moja kwa moja akaeleka katika jengo la kuhifadhia maiti. Akamshusha Tomas ndani ya gari huku akiwa amefungwa pingu za mikononi na miguuni akiwa na nyororo ndefu iliyo muwezesha kupiga hatua fupi fupi. Akamshika mkono huku akiichomoa bastola yake kiunoni.
“Nahitaji kuziona zile maiti zilizo letwa na vijana wangu”
RPC alimuambia muhudumu wa jengo hilo. Wakaongozana na muhudumu huyo hadi kwenye mafriji makubwa ya kuhifadhia maiti. Tomas japo ni mjanja sana, ila katika maisha yake yote hakuwahi kuingia katika jengo la kuhifadhia maiti(Mochwari). RPC akaagiza maiti hizo kutolewa nje ya mafriji hayo huku zikiwa zimefunikwa. Muhudumu huyo ambaye macho yake ni mekundu sana kutokana na uvutaji wa bangi ili kutoa woga wa kuhudumia maiti hizo akasimama pembeni yao huku akiwatazama. RPC akaifunua maiti moja na akamuonyesha Tomas maiti ya Selemani D iliyo chakaa kwa kupigwa risasi.
“Hawa jana tu walikuwa hai, wakisherekea pesa nyingi walizo zivuna kwa kumteka nabii Sanga. Ila sasa hivi wapo hapa hawajitambui. Wewe upo hai ila hii bastola yangu ina weza kukulaza na wewe hapa na ukajumuika na hawa wezako. Niambie ni wapi wezako walipo mpeleka nabii Sanga la sivyo, utaungana nao na wewe utaingizwa kwenye jokofu lile pale ukiwa maiti”
RPC alizungumza huku akimuwekea Tomas bastola ya kichwani na kumfanya Tomas kuanza kutetemeka mwili mzima huku akiona mwisho wa maisha yake sasa umefika, tena ana fia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.
                            ITAENDELEA
Haya sasa, Tomas amekata tamaa ya kuishi, hajui ni wapi alipo nabii Sanga. Magreth amelala masikini na kuamka tajiri, huku maisha yake yakiwa yamebadililika. Je maombi ya mrs Sanga yana weza kutenda miujiza ya kumtoa Tomas mikononi mwa polisi. Nini kitatokea? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 12
 
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )