Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 15, 2020

Wafanyakazi wanne wa Ikulu ya Rais wa Kenya Wapata Corona....Maambukizi Yapindukia 3,727, Vifo 104

juu
Wafanyakazi wanne wa Ikulu ya rais nchini Kenya wamepatikana na virus vya corona.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu Kanze Dena, wafanyakazi hao waligunduliwa wameambukizwa COVID-19 baada ya kufanyiwa uchunguzi Alhamisi, Juni 11.

Maafisa hao walioambukizwa wamelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako wanaendelea kupata matibabu .

Msemaji wa Ikulu amewahakikishia Wakenya kuwa Rais Kenyata na familia yake wake wako salama na wamethibika kutokuwa na maambukizi ya corona.

Kufikia sasa Kenya ina jumla ya watu 3,727, walioambukizwa virusi vya corona kufuatia ongezeko la wagonjwa wengine wapya 133.

Katika taarifa za kila siku kuhusu muenendo wa ugonjwa wa corona nchini Kenya, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amesema kuwa wagonjwa 33 waliokuwa wamelazwa hospitali wameruhusiwa kuenda nyumbani katika kipindi cha saa 24 na kufikisha 1,286 jumla ya watu waliopona ugonjwa wa corona huku vifo vikifika 104
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )