Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 1, 2020

Wagonjwa Wa Corona Tanzania Wazidi Kupungua....Dar Es Salaam Wabaki Wanne Tu

Idadi ya wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona nchini Tanzania imezidi kupungua ambapo sasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam wagonjwa wamebaki wanne tu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza katika ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mkoani Tanga, ambapo ameongeza kuwa mikoa mingine haina wagonjwa kama vile Pwani na Mwanza.

Akitoa mchanganua wa wagonjwa hao waliopo Dar es Salaam amesema kuwa katika Hospitali ya Amana kuna wagonjwa watatu, na mmoja yupo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.

 
“Mkoa wa Tanga hakuna Mgonjwa hata Mmoja Kituo kimefungwa, DSM katika Hospitali ya Amana wamebaki 3, Mloganzila 1, Kibaha hatuna mgonjwa, Mwanza hatuna mgonjwa jambo la kusisitiza ni kuwa Corona bado ipo tuendelee kujikinga, na mimi nilisema pale Ikulu Dodoma katika Uwaziri wangu sikuwahi kupitia kipindi kigumu kama hiki cha Corona kwakweli nilihenya” amesema Waziri Ummy.

Akieleza mchakato mzima wa kupambana na virusi hivyo vinavyosababisha homa ya mapafu, Ummy Mwalimu amesema kuwa kilikuwa kipindi kigumu zaidi kwenye uwaziri wake, lakini anamshukuru Mungu kwa namna Tanzania ilivyofanikiwa kukabiliana na virusi hivyo vinavyoendelea kuisumbua dunia.

Kwa upande wake Waziri Kassim Majaliwa amempongeza Ummy Mwalimu kwa namna alivyosimama katika nafasi yake, na kwamba ameonesha kuwa yeye ni mwanamke wa shoka.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )