1.
Jopo
la mapitio ya viashiria vya uchumi mpana linalohusisha Mawaziri wa SADC wenye
dhamana ya Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu, walikutana kwa njia ya
mtandao tarehe 15 Julai 2020.
2.
Dhumuni
la mkutano huo ambao umefanyika kwa njia ya mtandao lilikuwa ni kupitia hatua
iliyofikiwa na nchi wanachama kuhusu mafanikio yaliyofikiwa kuelekea malengo ya
uchumi mpana yaliyokubaliwa pamoja na kubainisha changamoto za mwelekeo wa
kiuchumi katika kanda na kushauri hatua za kisera za kukabiliana na changamoto
hizo. Wakati huo huo, jopo limepokea taarifa kuhusu athari za janga la COVID-19
kwa nchi wanachama wa SADC pamoja na taarifa ya utekelezaji wa hatua za kufikia
malengo ya uchumi mpana.
3.
Jopo
pia lilipitia na kujadili taarifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo hii ni mara ya pili kwa nchi hizi mbili
kufanyiwa mapitio tangu mfumo wa SADC wa nchi moja kuifanyia tathimini nchi
nyingine kuzinduliwa mwezi Mei 2013, Maputo, Jamhuri ya Msumbiji.
4.
Jopo
lilibaini yafuatayo:-
Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo
4.1
Katika
miaka michache iliyopita, uchumi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umekuwa
ukiimarika, na hivyo kuiwezesha nchi kufikia malengo ya msingi na upili (primary
and secondary targets) yaliyokubaliwa na nchi wanachama.
4.2
Ukuaji
wa Pato la Taifa uliimarika kutoka asilimia 2.4 mwaka 2016 hadi asilimia 3.7
mwaka 2017 na asilimia 5.8 mwaka 2018, lakini ulipungua na kufikia asilimia 4.6
mwaka 2019 hususan kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa madini uliopelekea kuzorota
kwa bei ya bidhaa.
4.3
Mfumuko
wa bei ulishuka kwa kasi na kufikia asilimia 7.2 mwaka 2018 na asilimia 4.6
mwaka 2019 na inategemewa kufikia asilimia 5.0 mwaka 2020.
4.4
Wakati
huo huo, mfumo wa usimamizi wa malipo taslim umewezesha Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo kuwa na ziada kwenye bajeti ya asilimia 0.2 ya pato la taifa katika
kipindi cha mwaka 2016 na 2018, na kupungua kufikia nakisi ya asilimia 0.2 ya
pato la taifa kwa mwaka 2019.
4.5
Mwaka
2019, deni la taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilifikia asilimia 13.3
ya pato la taifa, uwiano ambao upo ndani ya lengo lililowekwa na nchi wanachama
wa SADC usiozidi asilimia 60 ya pato la taifa.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
4.6
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutekeleza mapendekezo ya Jopo la Mapitio la
Viashiria vya Uchumi Mpana kutokana na mapitio ya awali yaliyofanyika mwaka
2017.
4.7
Hivyo,
uchumi wa nchi ulishuhudia ukuaji wa uchumi wa wastani wa asilimia 6.9 katika
kipindi cha mwaka 2016 – 2018 ambao unaendana na shabaha ya Jopo la viashiria
vya uchumi mpana la SADC wa angalau asilimia 7.
4.8
Kiwango
cha Mfumuko wa bei kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilikua wastani wa
asilimia 4.4 kwa miaka minne iliyopita, ambapo kimebakia ndani ya shabaha za
SADC ya asilimia 3 – 7 na chini ya shabaha ya muda wa kati ya asilimia 5.
4.9
Nakisi
ya bajeti kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliongezeka katika kipindi cha mapitio kutoka asilimia 1.4
ya pato la taifa mwaka 2016 hadi asilimia 2.5 mwaka 2018 na kuimarika hadi kufikia
asilimia 2.3 mwaka 2019. Aidha, deni la Serikali lilifikia wastani wa asilimia
40 ya pato la taifa kati ya mwezi Juni 2016 na Juni 2019, uwiano ambao uko ndani
ya ukomo uliowekwa na nchi wanachama wa SADC wa asilimia 60.
5.
Jopo
lilijadili na kuidhinisha taarifa na mapendekezo ya kisera ya timu ya wataalam kwa
ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile,
Jopo liliridhika na utayari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika kutekeleza mapendekezo hayo.
6.
Katika
kuhitimisha, Jopo liliipongeza Falme ya Eswatini na Jamhuri ya Msumbiji kwa
kuifanyia mapitio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya
Madagascar kwa kuifanyia mapitio Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
7.
Jopo
lilikubaliana kuwa nchi za Angola, Namibia, Shelisheli na Zimbabwe zitakuwa
nchi wanachama zitakazofuata kufanyiwa mapitio katika kipindi cha mwaka 2020/2021.
8.
Jopo
lilitoa shukran zao za dhati kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa
SADC, kwa maandalizi mazuri yaliyofanywa wakati wa mkutano.
Sekretarieti ya SADC
15 Julai 2020
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )