Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, July 10, 2020

Mfanyakazi Wa Ndani Auawa Baada ya Kuwaua Kwa Mapanga Watoto Wawili wa Bosi Wake

juu
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MFANYAKAZI wa kazi za ndani mwanaume,Yasin Abdala (35), Kitongoji cha Kivungwi Kwazoka ,Kata ya Vigwaza Chalinze,Bagamoyo mkoani Pwani ameuwawa na wananchi wenye hasira kali baada kuwauwa watoto wawili wa bosi wake ,kwa kuwakatakata mapanga. 
 
Aidha marehemu pia amemjeruhi mama wa watoto hao Sada Salehe (28) kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa kituo cha afya Mlandizi kwa matibabu zaidi
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa alieleza ,tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Julai 9  nyumbani kwa Wema Senzie.
 
Alisema, mtuhumiwa ameuwawa na wananchi waliokwenda kumkamata baada ya kukimbia alipokuwa amehifadhiwa kwenye ofisi ya Kijiji.
 
Wankyo ,aliwataja Watoto hao aliowaua ni Abubakary Makolo (6) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Kwazoka na mdogo wake Rehema Makolo (5) mwanafunzi wa shule ya awali Kwazoka.
 
“Mtuhumiwa baada ya kukamatwa alihifadhiwa ofisini hapo kwa ajili ya kupelekwa kwenye vyombo vya sheria lakini alivunja mlango na kukimbia na walipomkamata walimshambulia kwa silaha za jadi na kusababisha kifo chake,” alisema Wankyo.
 
Wankyo alibainisha, chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa na polisi ila awali kabla ya tukio hilo mtuhumiwa alikuwa na ugomvi na mama wa watoto hao.
 
Miili ya marehemu imehifadhiwa  kwenye kituo cha afya Mlandizi ,kusubiri taratibu za mazishi.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )