Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka
viongozi wapya walioapishwa leo kuimarisha ushirikiano mzuri na
watendaji waliopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza ufanisi mzuri
katika utendaji kazi wa kuleta maendeleo ya kujenga nchi.
Wito huo ameutoa leo Ikulu ya Jijini Dodoma wakati wa kuwaapisha viongozi wapya walioteuliwa hivi karibuni.
Aidha
Rais Magufuli, amesema kuwa ufanisi mzuri wa watendaji hao katika
nafasi zao ndio itakuwa chachu ya kuendelea kuinua uchumi wa kati kutoka
hapo ulipo na kukua zaidi.
“Nendeini
mkachape kazi ya kuwatumikia watanzania kwa kumtanguliza Mungu ili
kuweza kufanikiwa katika kutekeleza majukumu yenu”, amesisitiza Rais
Magufuli. (PICHA: IKULU)
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )