Rais Magufuli amempongeza Dk. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Malawi.
Kupitia
ukurasa wake wa Twitter; Rais Magufuli amesema, “Nakupongeza Dkt.
Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi.
“Kwa
niaba ya Serikali na Watanzania wote, naahidi kuendeleza uhusiano wetu
wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi
na ustawi wa jamii. Hongera sana Mhe. Rais,” amesema.
Chakwera amechaguliwa na Wamalawi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 23 Juni 2020 kwa kupata asilimia 58 akimshinda Rais aliyekuwa madarakani Peter Mutharika.
Uchaguzi huo ulifanyika baada ya ule wa awali wa Mei 2019 kufutwa na mahakama Februari 2020 baada ya kubaini ulikuwa na dosari.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )