Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa katibu wa Itikadi na uenezei wa Chama hicho, Humprey Polepole kimetoa utaratibu na ratiba kamili itakayoohusisha mchakato wa uchukuaji fomu kwa wagombea wa udiwani/masheha na wabunge/wawakilishi kupitia tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.
Utaratibu huo umetolewa leo Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma
Kupitia mkutano huo Polepole ametangaza Kanuni na baadhi ya maboresho yaliyofanywa kwenye Katiba ya CCM ili kupanua wigo wa demokrasia kupitia Mkutano Mkuu wa CCM uliomalizika wiki iliyopita kwa ajili ya uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Amesema kanuni ya uchaguzi na uteuzi inazungumzia makatazo fulani fulani kuhusiana na mambo ya kulalamikia ambayo hayahusiani na rushwa.
Ametoa mfano wa matendo hayo kuwa ni matumizi ya mabango, vipeperushi vikiwemo vya kwenye mitandao au mabango. Polepole amesema vitendo hivyo haviruhusiwi na kwamba ni kosa, kwani kufanya hivyo ni kuanza kampeni kabla ya wakati.
Amesema makada wa Chama hicho ambao watabainika kufanya hivyo wataadhibiwa na Kamati ya Siasa inayohusika.
Pia Polepole amezielekeza Kamati za Siasa za Wilaya na majimbo kuwaelekeza wale ambao walikuwa tayari wamechapisha vipeperushi na mabango kuwaonya na kuwaelekeza kuyaondoa.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )