Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, July 3, 2020

TAKUKURU Mkoani Shinyanga Wamtia Mbaroni mfanyabiashara Joseph Tasia akiwa na doti 600 za vitenge vyenye nembo ya CCM

juu
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga inamshikilia Joseph Jonas Tasia mkazi wa Mwasele Mjini Shinyanga kwa kukutwa na doti 600 za vitenge vyenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Takukuru imesema, vitenge hivyo vya kawaida, vinadaiwa kutaka kutumika kushawishi wapiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa tarehe 3 Julai 2020 na Mkuu wa Takukuru, Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa kupitia taarifa yake kwa umma.

Mussa amesema, tarehe 29 Juni 2020 saa 3 usiku, katika mtaa wa Mwasele B nyumba ya Tasia, walimkuta na doti hizo za vitenge vikiwa vimehifadhiwa nyumbani kwake jambo ambalo linaashiria vilikuwa vinaandaliwa kutumika katika kufanya ushawishi kwa wapiga kura.

Amesema, uchunguzi walioufanya, wamebaini, Tasia ambaye ni mfanyabiashara wa usafiri wa magari madogo ‘taxi’ hana duka na wala hafanyi biashara ya kuuza vitenge.

“Katika mahojiano na maafisa wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, ameshindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na mzigo husika na hata nyaraka za manunuzi ya mzigo huo alizowasilisha hazijitoshelezi na hivyo kuongeza mashaka juu ya uhalali wa vitenge hivyo,” amesema Mussa.

Amesema, uchunguzi wa kina bado unaendelea ili kubaini iwapo vitenge vilikuwa ni kwa ajili ya kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa katika uchaguzi ujao au ni kwa ajili ya kufanya biashara msimu huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )