Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, July 14, 2020

Waziri wa wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala Arejesha Fomu Ya Kuomba Kuteuliwa Kuwania Ubunge Wa Nzega Vijijini

juu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala amekuwa mwanachama wa kwanza wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini.

Dkt. Kigwangalla alirejesha fomu hiyo leo ikiwa ni siku ya kwanza tangu zoezi la kuchukua fomu kwa wanachama wa CCM lilipofunguliwa.

Alisema anaomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM ili aweze kushirikiana na wachamama wa CCM katika Jimbo la Nzega Vijijini na wadau wa maendeleo katika kutatua matatizo yaliyobaki ya uboreshaji wa miundombinu.

Dkt. Kigwangalla alisema katika kipindi cha miaka mitano ndani ya jimbo hilo kumekuwepo na mafanikio makubwa ikiwemo kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria, usambazaji wa umeme wa REA kwa wananchi na ujenzi wa miundombinu ya afya.

Alisema kama akipewa fursa nyingine atajitahidi kushirikiana na Serikali na wakazi wa Jimbo hilo katika kuhakikisha wanarekebisha miundombinu ya barabara.

MWISHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )