Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 11, 2020

Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumchinja Mtoto Wake wa Kambo

juu
Jeshi  la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Ayoub John (38), mvuvi katika kisiwa cha Chakazimbwe wilayani Muleba kwa tuhuma za kumuua kwa kumchinja mtoto wake wa kambo Aidan Greyson (3).

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, alisema jana kuwa mtoto huyo wa kiume anadaiwa kuuawa na baba yake wa kambo usiku wa kuamkia Agosti 8, mwaka huu.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi baina ya John na mke wake ambaye ni mama wa mtoto huyo, Mektirida Nestory (27). Kutokana na ugomvi huo, alisema Nestory alikimbia kwa kuhofia maisha yake na kumwacha mtoto ndani ya nyumba.

"Kulizuka ugomvi mkubwa kati ya wanandoa hawa baada ya baba mwenye nyumba kurejea nyumbani usiku akiwa amelewa. Walipigana na mama akaamua kukimbilia kwa jirani na kumwacha mtoto huyo aliyemzaa na baba mwingine kabla ya kuolewa na mtuhumiwa. Aliporejea asubuhi alikuta mtoto ameuawa," alisema.

Kamanda huyo alisema mama alikuta mtuhumiwa huyo akiwa amelala kitandani na mtoto huyo ambaye tayari alikuwa amekwishamchinja, akakimbia huku akipiga kelele kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kumkamata kisha kumpeleka polisi.

Alisema chanzo cha ugomvi huo uliosababisha kifo cha mtoto ni baba kumtuhumu mke wake kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )