Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, August 14, 2020

Bashungwa Atembelea Viwanda Vya Saruji Kuhakikisha Vinazalisha Kwa Uwezo Uliosimikwa.

juu
Ikiwa ni Mwendelezo wa ratiba ya ziara za Wizara ya Viwanda na Biashara za kutembelea na kukagua viwanda vya saruji nchini.

Leo 14 Augusti 2020, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe kutembelea na kukagua utendaji Kazi wa Kiwanda cha saruji Camel Cement kilichopo Mbagara jijini Dar es salaam.

Katika ziara hiyo Waziri Bashungwa amebainisha lengo na Madhumuni ya kutembelea viwanda vya saruji nchini ni baadaa ya kupata fursa na maombi ya uhitaji wa saruji kutoka nchi jirani za uhitaji wa saruji kutoka Tanzania.

Waziri Bashungwa ameanza kwa kuvipongeza viwanda vya saruji nchini kwa kazi kubwa ya uzalishaji wa saruji inayotosheleza mahitaji ya nchi na nyingine kusafirishwa nje ya nchi na sasa mkakati wa wizara ni kuhakikisha viwanda vyote vya saruji vinazalisha kufikia uwezo wao uliosimikwa na kama kuna changamoto zinazozuia viwanda visifikie uzalizaji uliosimikwa ziweze kutatuliwa mara moja maana ndio kazi ya serikali kwa wawekezaji wote nchini.

Aidha, Waziri Bahungwa amevihakikishia viwanda vyote nchini juu ya tatizo la umeme kuwa mpaka sasa mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere upo katika hatua nzuri na muda si mrefu tatizo hilo litakuwa hisitoria na tutakuwa na uhakika wa umeme wa kutosha na unaopatikana muda wote ili  dhima ya Rais John Pombe Magufuli ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya yenye uchumi wa Viwanda iweze kutimia na kutekelezwa kiurahisi.

Sambamba na hayo, Waziri Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe kukutana na wenye viwanda vya saruji ili kuweka mkakati wa kujenga viwanda vya saruji kwenye mikoa ya kati na kanda ya ziwa au kati maana sio lazima kujenga kiwanda sehemu ambapo zinapatikana malighafi zote

Bashungwa amemaliza kwa kuwakaribisha wawekezaji wapya na waliopo kuwekeza kwenye viwanda vya saruji katika mikoa ya kati na kanda ya ziwa maana teknolojia na miundombinu vimeboreshwa na vinaruhusu mwekezaji kujenga kiwanda mkoa wowote maana malighafi zinaweza kufika tena kwa bei rahisi na rafiki kwa wawekezaji kwa sababu kuna mikoa iko mbali na viwanda vilipo mpaka umbali wa kilometa 1000 na baada ya kusafirisha saruji sasa tusafirishe malighafi ili viwanda vijengwe huko huko.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe kutembelea na kukagua utendaji Kazi wa Kiwanda cha saruji Camel Cement kilichopo Mbagara jijini Dar es salaam.
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )