Mkutano Mkuu wa chama ACT-Wazalendo, umewateua Bernard Membe na Maalim Seif Sharif Hamad kuwa wagombea urais wa Tanzania na Zanzibar.
Membe na Maalim Seif wameteuliwa leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 katika mkutano mkuu huo uliofanyikia ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Joran Bashange amesema, wajumbe walikuwa 428 ambapo waliopoga kura kumteua mgombea urais wa Tanzania walikuwa 420.
Bashange amesema, Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania amepata kura 410 sawa na asilimia 97 huku kura kumi zikimkataa.
Nafasi ya mgombea urais wa Zanzibar, Bashange amesema, waliopiga kura walikuwa 420 ambapo kura 419 ni za ndio sawa na asilimia 99.6 na kura moja imemkataa.
Hii ina maana kwamba, Maalim Seif Sharif Hamad atakwenda kuchuana na wagombea wa vyama vingine akiwemo Dk. Hussein Ali Mwinyi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pia, Membe atakwenda kuchuana na wagombea wengine wakiwemo Rais John Pombe Magufuli wa CCM na Tundu Lissu wa Chadema
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )