Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, August 13, 2020

Robert Kaseko: Kwani Nini Watanzania Tunapaswa Kumchagua Rais Magufuli Tena Kwa Miaka Mingine Mitano ( 2020 - 2025 )

juu
Mwandishi Mmoja wa Vitabu  Mashuhuli  Duniani  na Mbobezi wa Masuala  ya Uongozi  Peter Ferdinand  Drucker  ambaye ni Marehemu kwa sasa, Kupitia Kazi yake ya Kuelimisha Jamii  aliwahi kusema, NANUKUU;  “Effective leadership is not about making speeches or being liked; leadership is defined by results not attributes”  akimaanisha ya Kwamba  Uongozi  uliotukuka sio  kutengeneza Hotuba nzuri zenye kukonga mioyo ya watu  au kupendwa bali Uongozi mzuri hutazamwa kwa Matokeo  na sio sifa.

Aidha nimemnukuu Mwandishi mwingine Ngunguli wa Vitabu John Maxwell ambaye pia aliwahi kusema NUKUU: “ A leader is one who knows the way, goes the way and shows the way”  akimaanisha Kiongozi mzuri ni Yule anayejua njia, anayokwenda na kuonyesha njia hiyo. Huwezi kuwaongoza Wasafiri wengine kwenda kusikojulikana.  Rais Magufuli anajua vyema Taifa letu linakopaswa  kuwa na Njia gani za kutufikisha huko.

Kwa Kipindi Kifupi sana yaani Miaka ndani ya Miaka Mitano tu Rais Magufuli amefanya Makubwa ambayo tulizoea kuona yakitekelezwa kwa Miaka na Miaka baada ya ahadi. Rais Magufuli akiahidi anatimiza na kitu kinaonekana kabla ya muda alioahidi kumalizika. 

YAPO MENGI YA KUJIVUNIA  CHINI YA RAIS MAGUFULI ( Twende pamoja chini hapa ).

Katika Kipindi Cha Miaka Mitano iliyopita ( 2015 -2020 ) Watanzania tumemuelewa Vizuri Kiongozi wetu, Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwa miaka Mitano iliyopita Tumeshuhudia  Rais John Pombe Magufuli akiendelea Kuwa Mfuasi Mzuri wa  Falsafa za Mwalimu Julius Nyerere ambaye Kupitia Dira ya Uongozi wake,  alisisitiza sana Kujenga Taifa la Kijamaa na Kujitegemea.

 Niendelee Kwa Kusema Kuwa  Rais Magufuli Mara baada ya kuingia tu Madarakani ili Kujenga Taifa la Kujitegemea Kiuchumi alifanya yafuatayo na kuendelea kuyasimamia Kikamilifu; Ameboresha Ukusanyaji  Mapato ya serikali yatokanayo na Kodi  Kutoka Bilioni 850 Mwaka 2015  hadi  Kufikia Trilioni 1.3 ( Disemba 2019 )  Fedha za Kitanzania na Kwa Mapato yasiyo ya Kodi Rais Magufuli amefanikiwa kwa Kiasi Kikubwa Kuboresha Ukusanyaji wake  na Kuongezeka Kutoka Chini ya Bilioni 688 mwaka 2014/2015 hadi Kufikia Trilioni 2.4  Fedha za Kitanzania Mwaka 2018/2019

 Aidha Rais Magufuli pia amefanikiwa sana Katika  kudhibiti Matumizi yake na  Kwa Kiasi kikubwa   ameelekeza fedha  hizo kuwahudumia Watanzania Kwa kuwaletea Maendeleo Katika Sekta zote. Rais Magufuli amefanikiwa Kwa Kiasi Kikubwa Kuimarisha Utendaji Kazi Serikalini, Maadili na Nidhamu Kwa Watumishi wote wa Serikali ( UMMA ) na Katika hili hakusita Kuchukua hatua za kinidhamu hadharani  Kwa Watumishi Walioshindwa Kufanya Kazi kwa Weledi, Nidhamu, Maarifa na Uadilifu.

Rais Magufuli amevikoleza kweli kweli Vita dhidi ya wanaohujumu Uchumi wetu na Mafisadi ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mahakama ya Uhujumu Uchumi. Tumeshuhudia akiokoa  Fedha za Watanzania  Kutoka mbalimbali  walioburuzwa Katika vyombo husika.

Rais Magufuli toka ameingia madarakani mwaka 2015 alituahidi Kulinda Raslimali za Taifa letu ili kuhakikisha Urithi wa Raslimali tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu zinabaki Kuwanufaisha Watanzania wote na hapa ningependa kuwakumbusha Watanzania Kwa kurejea  katika lile Sakata la makinikia na Madini yetu kama mfano mmoja wapo.

Mosi kabisa, Mageuzi Makubwa sana yamefanyika  Ikiwa ni pamoja na Kuanzisha Wizara Mahsusi ya Madini, Kudhibiti Utoroshaji  na Usafirishaji wa Madini ghafi nje ya Nchi, Rais Magufuli ameanzisha Masoko ya Madini Kila Mkoa ambapo Kupitia hili Mapato  yatokanayo na Madini sasa yamekuwa na yanaonekana wazi. Serikali ya Rais Magufuli kupitia Bunge la JMT ilitunga na kupitisha Sheria ya Kulinda Rasilimali za Taifa ya Mwaka 2017 (  The Natural Wealth and Resources Permanent Sovereignty Act, 2017 ) Ikiwemo Madini.

 Kupitia Sheria hii, tumeshuhudiwa Kwa mara ya Kwanza  Watanzania wanamiliki Rasilimali zao kwa Nguvu za Kisheria Kama akina Saniniu Laizer😅 Mzee wa Tanzanite.

Ni kupitia Sheria hiyo pamoja na Jitihada za Rais  Magufuli na Serikali yake, wale Waliokuwa wanatunyonya “Mabeberu"  Walisalimu Amri na Kukubali Kutulipa Watanzania Malipo ya Fidia ya *Dola za Kimarekani Milioni Mia Tatu ( us-dollars 300 Millions ) ambazo Kampuni ya Barrick  ilikubali Kutulipa Kufuatia Majadiliano na Makubaliano na Tayari Dola za Kimarekani Milioni Mia Moja ( us –dollars 100 Millions ) tumekwisha lipwa.

 Mafanikio mengine Kupitia Makubaliano ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick*  ni pamoja na Kuanzishwa  kwa Kampuni ya Twiga Minerals Company  ambayo Serikali yetu inamiliki 16%  na Kampuni ya Barick 84% .

Watanzania tunayo mengi sana  ya Kujivunia Kama Taifa linalohitaji Kusonga Mbele  Kimaendeleo, Kiuchumi na Kidemokrasia pia.

Kwa Uchache tu, nakukumbushia Machache Miongoni Mwa Mengi aliyoyafanya:

• Sisi watu wa Arusha ametuletea Miradi Mkubwa wa Maji: Bilioni 520 Arusha Jiji, Mradi wa Maji Chanzo toka Mto Simba Kilimanjaro Bilioni 16, Ujenzi na Upanuzi wa Barabara  Kuwa njia nne Kutoa  Ngaramtoni hadi USA River  ikiwemo zile za Mchepuko / Mzunguko ( By-Pass ) ambazo zimekamilika zaidi ya Bilioni 164, Tumejengewa Hospitali  Mpya  za Wilaya  ya Longido ( Bilioni 2 ), H/Wilaya Karatu Bilioni 1.5, H/ Wilaya Ngorongoro ( Bilioni 1.8 )  na H/Wilaya Arusha ( Bilioni 1.5 ) Pamoja na Kuboresha Hospitali za zamani.

• Ununuzi wa Ndege Mpya 11 Kwa fedha zetu za ndani sio mkopo, yaani CASH PAYMENTS ( Boeing 787-8 Dreamliners ziko 2, Airbus 220-300 ziko 2, Bombadier Dash 8  Q-400 ziko 4 na  nyingine Tatu kuja Miezi michache ijayo. Hapa Serikali ya Dkt. Magufuli imeboresha huduma ya Usafili wa Anga kupitia  Shirika  la  Huduma  ya  Usafirishaji Kwa  njia ya  Anga Tanzania      ( ATCL )ambapo Mapato yameongezeka na Utalii umeongezeka zaidi na Kuongeza Pato la Taifa.

• Ujenzi Mradi Mkubwa wa Uzalishaji  Umeme wa Mwl. Nyerere - Megawati 2115 ( Stieglers Gorge ) utakaogharimu  Pesa zetu za ndani Trilioni 6.5 ( Dola za Kimarekani Bilioni 2.9 ) hadi kukamilika Kwake na Kazi inaendelea vizuri sana.
Tanzania ya Viwanda Ileeeeeee…

• Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa  ya Treni ya Umeme ( SGR ) Kutoka  Dar es salaam hadi Mwanza. Maendeleo ya Mradi wa Kipande cha Kutoka  DSM-Morogoro na Kutoka Morogoro hadi Makutupora  Dodoma utagharimu Trilioni 7.062  fedha zetu wenyewe kwa kodi zetu.  Kipande cha Mwanza –Isaka-Dodoma Maandalizi yanaendelea vizuri. Aidha sisi watu wa Arusha tumeshuhudia Ukarabati Mkubwa Reli za zamani za Kutoka  Dar es salaa-Tanga-Arusha na Kurejeshwa Kwa huduma za Usafiri wa Treni Chini ya Rais Magufuli ambazo zaidi zilikufa miaka 18 iliyopita, pia Ukarabati wa ile Reli ya Kutoka Dar es salaam hadi Isaka. Tukumbuke pia Miradi yote hii imetengeneza Ajira kwetu sisi vijana, wazee na wanawake pia.

• Rais Magufuli hakuwasahau wana Dar es salama. Kawapelekea Miradi ya Kutosha;

 Miradi Mikubwa ya Ujenzi wa Madaraja na  Barabara za Juu  kama: Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu Ubungo ( Ubungo Interchange Flyover (  zaidi ya Bilioni 200 zimetumika ), Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu - Mfugale flyover  ( zaidi ya Bilioni 247  ), Mradi wa Salender Brigde  na Daraja la Majini Ziwa Viktoria  Busisi – Kigongo urefu wa Km 3.2 litakalo gharimu Bilioni 699 pesa za Kitanzania hadi kukamilika kwake, ujenzi unaendelea vizuri sana.

• Mpango wa Elimu Bila Malipo Kuanzia Shule Msingi hadi Sekondari ambapo Serikali ya JPM inatenga zaidi ya Bilioni 23 Kila mwezi ili kugharamia Elimu Msingi hadi Sekondari.

• Rais Magufuli ametimiza ndoto  ya  Baba wa Taifa Hayati  Mwl. JK Nyerere ya Mpango wa Kuhamishia  Serikali Dodoma. Dodoma sasa inapendeza, vijana wamepata ajira na Maendeleo Mkoa wa Dodoma sio suala la kuuliza Mwenye Majicho atizame mwenyewe.

• Mpango wa Kujenga Vituo vya Afya Kila Kata Nchini Kote Kwa Maeneo yasiyokuwa na Vituo vya Afya. Kwa hakika Hapa Rais Magufuli tunamshukuru sana, sisi watu wa Mkoa wa  Arusha tumebahatika kuwa watu wa mwanzo kabisa kuanza kupata Vituo Vya Afya Vipya  14 Mpaka sasa vyenye thamani ya Bilioni 6.1 Fedha za Kitanzania  kati ya vituo vipya vya afya  360 vinavyojengwa Nchini Kote  Kupitia mpango huu  kabambe .

• Rais Magufuli pia ameweza Kujenga Hospitali  Mpya za Wilaya  Katika Halmashauri 67 Nchini Kote.

• Uboreshaji wa Viwanja vya Ndege ikiwemo Jengo Jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ( JNI ), Mradi uliogharimu Bilioni 722 Fedha zetu za ndani. Sambamba na hili tunakumbuka pia Ununuzi na Ujenzi wa Mifumo ya Kuongozea Ndege Katika Viwanja vya Ndege vya JNIA Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro na  Songwe Kwa gharama ya Bilioni 67.3 Fedha zilizotolewa na Serikali ya Rais Magufuli.

• Hatuwezi Kusahau namna Rais Magufuli alivyotusambazia Nchini Kote Miradi ya Ujenzi wa  Mabarabara  Kwa Kiwango cha Lami. Watu wa Arusha ni Mashahidi, Dar es salaam ni Mashuhuda pia namna Rais Magufuli alivyoruhusu Mabilioni ya Pesa Kuondoa Misongamano na Mafoleni Jiji la Dar es salaam.

Ndugu zangu ni Mengi ya Kujivunia Kutokana na Uongozi wa Rais Magufuli. Nimeshindwa Kuyaandika yote maana ni Mengi sana.  Rais Magufuli ametuinua pakubwa sana, bado ni Kiongozi sahihi kwetu Kama Taifa.
 
Robert PJN Kaseko
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya H/Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )