Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 4, 2020

Serikali Kuongeza Siku Mbili Za Kufanyika Maonesho Ya Kilimo Nanenane

juu
Serikali imetangaza kuongeza muda wa siku mbili za kufanyika kwa maonesho ya Kilimo ya Nanenane kote nchini ikiwa na lengo la kuwezesha wakulima, wafugaji , wavuvi  na wananchi wengi zaidi kufika kwenye viwanja vya maonesho kujifunza kanuni bora za uzalishaji mazao, teknolojia mpya pamoja na fursa za masoko ya mazao yao. 

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet N.Hasunga leo alipongea na waandishi wa habari kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane Nyakabindi mkoani Simiyu. 

“Muda wa maonesho ya Nanenane ni siku nane.Hata hivyo, mwaka huu sherehe zimechelewa kuanza baadhi ya kanda. Kulingana na mahitaji ya sherehe hizi kitaifa kilele kitakuwa siku ya tarehe 08 Agosti, 2020. Hivyo,tumeamua kuongeza siku mbili ya Jumapili na Jumatatu ili wananchi ambao hawakupata nafasi wapate kushiriki “
alisema Waziri Hasunga 

Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane mwaka huu inasema “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”
Imetolewa na ;

Revocatus A. Kassimba
Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano Serikalini.
WIZARA YA KILIMO
 
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )