Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, August 15, 2020

Umeme na fursa za kiuchumi vijijini

juu
 Na Samirah Yusuph,Bariadi.
Wakati wanaendelea kutimiza ndoto ya serikali ya kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinapata umeme, wakala wa nishati vijijini (REA) wamejikita katika kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wote vijiji ili kuweza kuwainua ki uchumi.

REA imevuka malengo ya serikali ya kuhakikisha kuwa asilimia 85 ya vijiji vinafikiwa na nishati ya umeme ifikapo 2020 umeme, Ambapo tayari vijiji katika hatua ya tatu mzunguko wa kwanza (phase III round 1) wamefikia vijiji vipatavyo 9402.

Aelezea mafanikio mwenyekiti wa Bodi hiyo Wakili Julius Kilolo alisema kwamba, wanachokilenga ni kuhakikisha kuwa wanawashawishi wananchi wa hali ya chini ili kuhakikisha wanapata nishati hiyo kwa matumizi ya nyumbani pamoja na shughili za kilimo na ufugaji.

“tunajitahidi kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kuwashawishi ili nishati hii ikadilishe maisha yao hasasa katika shughuli za kilimo na ufugaji, katika awamu hizi tatu tumefikia wilaya na kata zote na tayari wananufaika na huduma zetu,” alisema Wakili Kilolo.

Aliongeza kuwa ifikapo tarehe moja mwezi wa saba 2025 tayari watakuwa wametoka katika kufikisha umeme ngazi ya kata na vijiji na watakuwa katika ngazi ya vitongoji na huko watavifikia vitongoji vyote na kuhakikisha kuwa huduma inakuwa bora.

Uhakika wa  wa upatikanaji  wa huduma.
katika kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inayopelekwa vijijini inakuwa na matokeo chanya katika kuinua uchumi wa wananchi waishio katika maeneo hayo, Mr Francis Songela mjumbe wa bodi ya REA alisema kuwa wanahakikisha ukaguzi mara kwa mara.

Alisema kuwa ukaguzi huo unakuwa unalenga kufuatilia hatua za ufundi, ili kuhakikisha umeme unakuwa haukatiki kila mara pamoja na kuhakikisha kuwa umeme huo unakuwa ni kwa matumizi yenye manufaa na sio kuwasha taa pekee.

“ tunashirikiana na serikali katika kulinda miundo mbinu ya umeme kama nguzo ili kuhakikisha kuwa hakuna shughuri za kibinadamu ambazo zinaweza kuleta athari katika shughuli za usafirishaji wa umeme,” alisema Songela.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha miundombinu inabaki salama, tayari wamekabidhi jukumu la ulinzi katika ngazi ya vijiji ili watendaji walio karibu na wananchi waweze kushirikiana nao katika kutoa elimu itakayo saidia kuwapa uelewa wa kutunza miundombinu hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa ufundi kutoka REA Eng.Jones Oluto alisema kuwa nishati ya umeme inamfikia mtu yeyote ambaye anauhitaji hata kama ni katika nyumba ya udongo, kwa kutumia kifaa kidogo chenye uwezo wa kupokea na kusambaza umeme nyumbani kwa gharama nafuu.

“ kifaa hiki kinaitwa UMETA ni kifaa ambacho kinapokea umeme kutoka kwenye mita na kusambaza ndani bila kuhitaji mlolongo mrefu wa usambazaji wa umeme ndani ya nyumba, kifaa hiki kinafungwa sehemu yoyote hata kama ni kwenye nyumba ya makuti au udogo na gharama yake ni ndogo sana,”  alisema Eng. Oluto.

Aliongeza kuwa kifaa hicho kinafanya kazi sawa na mfumo mkubwa wa usambazaji wa umeme ndani ya jingo na hiki ni rahisi sana kwa matumizi ya nyumbani hivyo hakutakuwa na hofu yoyote ya upatikanaji wa umeme kwa wananchi wenye nyumba za udongo na makuti.

Hali ya upatikanaji wa umeme mkao wa Simiyu.
 Meneja wa Tanesco mkoa wa Simiyu Khadija Abdallah alisema kuwa, umeme umewafikia ipasavyo wananchi na kuwa bado kuna namba ndogo sana ya vijiji ambavyo havina umeme ukilinganisha na vile vyenye umeme.

“ni jukumu la wananchi kutumia miundo mbinu ya umeme kuhakikisha inakuwa na manufaa kwao ili kukwepa utumiaji wa umeme kuwasha taa pekeake,” alisema Khadija.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha umeme unakuwa haukatiki mara kwa mara, wanazingatia ukaguzi wa mienendo ya usambazaji wa umeme ili kuhakikisha kuwa wanatatua kwa haraka changamoto zinazojitokeza.

Wananchi wananufaika vipi?
Kutokana na kupelekewa nishati ya umeme vijijini  wananchi wamekuwa na manufaa zaidi tifauti na hapo awali mbapo huduma nyingi zilipatikana mjini pekee kutokana na kutokuwa na umeme,

Baadhi ya wananchi wameeleza namna ambavyo wamenufaika na nishati hiyo kwa maeneo ya vijijini, kuwa ni pamoja na kuwafungulia fursa za kibiashara.

“Kwanza kabisa Umeme ni Nishati muhimu  sana katika maisha ya kila siku,Umenisaidia  kupunguza za  gharama hapa shuleni mfano Baada ya shule yangu kuwekewa umeme ambapo mimi kama Mwalim Mkuu msaidizi nilishauri kununua photocopy machine hivyo kuifanya shule yetu kua na mradi ambao umeisaidia jamii kupata huduma ya photocopy maeneo ya karibu tofauti na mwanzo iliwalazimu kwenda umbali  wa kilometa 9 kupata huduma hiyo” alisema Yonaza Lawrence Mndeme.

“Kwa Biashara ukiwa na umeme nyumbani kwako unaweza ukawa na friji ambayo utatengeneza hata barafu,maji au matunda utauza na kuongeza uchumi wako kwa wanawake wa vijijini na wao wanamsogelea mwanamke wa mjini sababu wameacha utegemezi wanatumia fursa ya umeme kuwafikia,” alisema Ephulaim Simeon

“ siku hizi watu hawasumbuki viwandani kila kitu kinafanywa kwa kutumia umeme mashine na zenyewe zinatumia umeme hata cherehani zinatumia umeme hutumii tena nguvu zako kukanyaga chelehani saivi unatumia akili yako tu ukweli umeme umeongeza fursa za kiuchumi nyingi sana,” aliongeza fundi Amina ambaye ni fundi cherehani.

umeme  tayari (UMETA) ni kifaa ambacho hakihitaji mtandao mkubwa wa umeme katika nyumba ili kusambaza umeme,kinafaa katika mazingira ambayo mtu hajafanya mtandao wa umeme katika nyumba yake na mazingira ya chumba kimoja au viwili.

Mwisho.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )