Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 11, 2020

Wafamasia watakiwa kujitathimini katika utendaji wao.

juu
Na Samirah Yusuph, Simiyu
Wafamasi katika mkoa wa Simiyu wametakiwa kujitathimi katika utendaji  wao, ili kuhakikisaha kuwa wanadhibiti matumizi ya dawa na vifaa tiba yasiyo sahihi katika vituo vyao vya kazi.

Akitoa agizo hilo mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka katika kikao kazi na wafanyakazi wa idara ya afya  amesema, wafamasia inabidi wajitume katika kutimiza majukumu yao na kwamba anatambua kuwa kwenye dawa kunachangamoto sana.

"Ni jambo baya sana kama kazi yako mwenyewe ukasahihishwa na mtu ambaye hana ujuzi nayo, ni aibu kwenu kusahihishwa na watu kutoka nje kwa nini msisahihishane nyinyi na kaloza changamoto zenu" alisema Mtaka

Aliongeza kuwa ni wazi kwamba anataarifa kuwa kuna wafamasia ambao hawafanyi kazi zao vizuri hivyo wanaipa hasara serikali jambo ambalo sio lengo la serikali kwa ujumla.

Akitoa taarifa ya Ukaguzi wa Mnyororo wa ugavi Dr. Festo Dugange, alisema kuwa lengo la kufanya ukaguzi ni kudhibiti matumizi mabaya ya dawa ili kiboresha wa vifaa katika vituo vya afya pamoja na kubaini hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

" Tumebaini uzembe uliopelekea ugumu wa kutambua uhalali wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa uliosababishwa na ubovu wa utunzaji wa kumbukumbu," alisema.

chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )