Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, August 5, 2020

Wagombea CCM Waliopita Kwa Njia za Udanganyifu Kuadhibiwa

juu
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitawaadhibu  watia nia waliopenya kwenye kura za maoni za kutafuta wagombea wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 2020, kupitia chama hicho kwa njia za udanganyifu ikiwemo rushwa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole,  wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM (OND) Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Jumatano, Agosti 5, 2020.

“Chama kimeona kiseme, tuko kwenye uchaguzi, mambo ni mengi na muda ni mchache, kila jambo tunalofanya lipo ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunatambua, kuheshimu na kufuata taratibu na sheria, tamaduni, desturi na taratibu za nchi yetu.

“Tulipenda wote walioomba dhamana wapate nafasi, waende kwenye kura za maoni wakapigiwe kura, viongozi wetu waliopewa dhamana ya kupiga kura wamefanya kazi nzuri sana, kwa uwazi na kwa demokrasia.

“Tunataka viongozi waaminifu, waadilifu wanaochukizwa na rushwa, mwaka huu tutawafundisha watu adabu, wagombea endeleeni kuwa watulivu kabisa, malamiko tunayaruhusu na viongozi wetu wanayapokea, tutawashangaza wanaodhani business as usual (mambo yanakwenda kama kawaida).

“Watu waaminifu na wanyenyekevu kwenye chama chetu nyie muwe na amani, hatutawangusha, lakini mliopiga mazonge tutafundisha watu adabu, sisemi maneno mengi, wakati mwingine ukitaka kumfundisha mtu adabu unamfundisha kwa sapraizi, wakatafute kazi nyingine,” amesema Polepole.

Vikao vya Kamati za Siasa za Mkoa za CCM kuwajadili wagombea hao vilivyoanza jana na vinatarajiwa kukamilika  leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020.

Vikao vya Kamati za Siasa za Mkoa za CCM vinafanyika baada ya mikutano mikuu ya CCM majimbo na wilaya kwa ajili ya kuchuja wagombea kufanyika.


Mikutano mikuu ya CCM ya majimbo kwa ajili ya hatua ya awali ya kupendekeza wagombea ilifanyika Julai 20 hadi 21, 2020 ikifuatiwa na vikao vya Kamati za Siasa za Wilaya vilivyofanyika tarehe 1 hadi 2 Agosti 2020.

Kwa upande wa wagombea wa udiwani, tarehe 6 Agosti 2020 Vikao vya NEC ngazi ya mikoa vitafanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa udiwani wakata na wadi pamoja na madiwani viti maalum.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )