Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 11, 2020

Waziri mkuu wa Lebanon Ajiuzulu kufuatia mripuko wa wiki iliyopita mjini Beirut

juu
Waziri mkuu wa Lebanon Hassan Diab ametangaza kujiuzulu kufuatia mripuko wa wiki iliyopita mjini Beirut. 

Kwenye taarifa yake fupi kupitia televisheni, waziri mkuu Diab alisema anachukua hatua hiyo ili aungane na watu wa Lebanon na kwa pamoja wapiganie mabadiliko. 

Rais Michel Aoun amekubaliana na hatua hiyo ya serikali kujiuzulu. 

Wiki iliyopita Diab alimlaumu mtangulizi wake kwa mripuko huo. 

Alisema wanasiasa wanatakiwa kuona aibu kwa sababu ufisadi ndio umesababisha janga hilo lililofichwa kwa miaka saba.

Baadhi ya mawaziri tayari walikuwa wamejiuzulu hapo kabla kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuibuka baada ya mripuko huo kutokea.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )