Na John Walter- BABATI
Mgombea mwenza wa Tundu Lissu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu, amehaidi kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara wote.
Alitoa ahadi hiyo jana Mjini Babati Mkoa wa Manyara wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Motel Papaa.
"Suala la kukadiliwa kodi kwa macho ni marufuku na maofisa wa TRA wengine hawajawahi kumiliki hata kibanda cha nyanya,"alisema Mwalimu
Aidha alisema mfanyabiashara hawezi kulinda biashara kwa kupigwa nyundo kichwani na maofisa wa bodi wasiokuwa waaminifu.
Mwanasiasa huyo alifafanua kuwa haki za wafanyabiashara zinatakiwa kulindwa kwa kuwa wanatunza kumbukumbu za biashara zao.
Alisema wengi wao wanafungua maduka yao kwa mazoea huku akiwahakikishia kufurahia kipindi cha uongozi wa Tundu Lissu.
Alitumia fursa hiyo kumuombea kura Lissu, wabunge na madiwani wa upinzani hasa wa Chadema.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )