Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, September 3, 2020

Mgombea Urais CCM Dr Magufuli Amuombea Kura Patrobas Katambi, Amtoa Hofu Stephen Masele .

juu
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Dr John Magufuli,  amewaomba wananchi wa Shinyanga kumpa kura mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi ambapo pia ameahidi kumtafutia kazi nyingine aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Stephen Masele .

Dr Magufuli ameyasema hayo leo  Septemba 03, 2020, wakati akizungumza na wananchi wa Shinyanga mjini katika mkutano wa kampeni za urais uliofanyika katika uwanja wa Kambarage.

“Yale mengine ya pembeni achaneni nayo, Katambi ni kijana nampenda mpeni kura, atawavusha, jana tu nimekutana na Masele aliyekuwa Mbunge wa hapa wala sina tatizo, mimi ni Rais nitamtafutia kazi nyingine, ukishakuwa Rais Makazi yapo mengi tu

“Masele nitamtafutia tu kazi ya kwenda kufanya, ukishakuwa Rais kazi ni nyingi, hata leo kuna nafasi ya Mtu mmoja anafanya hovyohovyo huko, Katambi ameacha Ukuu wa Wilaya Dodoma Makao Makuu kuja kuomba kura Shinyanga anawapenda, Katambi ukichaguliwa usibadilike kama wengine”-Amesema Rais Magufuli

Pamoja na hayo Magufuli ameelezea mipango ambayo anatarajia kuikamilisha katika Mkoa wa Shinyanga iwapo atarejea madarakani baada ya uchaguzi.

“Hapa Shinyanga tumetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospitali, zahanati na mradi mkubwa wa kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga ambapo itafika mahali tatizo la umeme litakuwa ni ndoto, kwani tumepeleka umeme katika vijiji 136 vya mkoa huu,” alisema huku akiahidi kukamilisha pia miradi mbalimbali ya barabara mkoani humo.
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )