Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, September 6, 2020

NHIF Yakanusha Taarifa Juu Ya Kusitisha Utoaji Huduma Baadhi Ya Dawa.

Na Faustine Gimu
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)umekanusha taarifa zinazoenea kwenye Mitando ya kijamii kuwa umesitisha utoaji wa baadhi ya dawa kwa watumiaji wahuduma hiyo

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma Sept 5,2020  katika ofisi za Mfuko huo Mkurugenzi Mkuu Benard kongaamesema taarifa hizo  zimeleta taharuki kwa wanachama wake

Amesema mfuko huo umejenga imani kubwa kwa wateja wake tangu kuasisiwa kwake mwaka 2001 kwa sasa una dawa 543 ambazo zikinyambulishwa zinafanya idadi ya  dawa 975  baada ya kuongeza kitita cha mafao mwaka 2016

Amewatoa hofu wanachama wa NHIF hapa nchini  na kuwataka kuendelea kutumia huduma hiyo na kutoa rai kwa wananchi kuepuka kutoa taarifa ambazo si sahihi.

Sept 4 mwaka huu zilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mfuko wa taifa wa bima ya afya nchini(NHIF)umezifuta dawa 138 kutoka orodha ya dawa zinazotolewa na mfuko huo kwa wanachama wake.
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: